Zenj FM

Viongozi wanaotumia vibaya mitandao wanahatarisha umoja wa kitaifa

28 July 2025, 5:23 pm

Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madai yaliotelewa na aliyekuwa balozi wa Cuba Humphire Polepole.

Na Mandishi wetu.

Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama, amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wanaotumia vibaya fursa ya mitandao ya kijamii jambo ambalo linaweza kusababisha kuvuruga umoja wa kitaifa kwa watanzania.
Mshangama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madai yaliotelewa na aliyekuwa balozi wa Cuba Humphire Polepole baada ya kudai wagombea wa urais wa CCM wamechaguliwa kinyume na katiba na kanuni ya chama.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama.

Amesema kwamba mkutano mkuu wa CCM umepitisha majina ya wagombea uliowateua Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuzingatia ibara ya 101 na 104 ya chama chao baada ya kuridhishwa na uongozi wao.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama.

Aidha mshangama amesema tatizo linalojitokeza hivi sasa baadhi ya viongozi hawakupita katika vyuo vya uongozi na kupata mafunzo kama ilivyokuwa siku za nyuma viongozi kuandaliwa na kupewa mafunzo katika vyuo vya maadili vya uongozi na jeshi la kujenga taifa.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama.

Amesema CCM inaviongozi wa kutosha wastaafu na kama watatumika vizuri mitafarouk inayojitokeza itaweza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya watu wanaokwenda kinyume na maadili na miko ya uongozi.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya uchumi na jamii Zanzibar, Abdulhamid Mshangama.

Kauli za balozi Polepole na mwenyekiti wa taasisi ya mwalimu nyerere Joseph Butiku zimezuwa mjadala mkubwa kuwa zinakwenda kinyume na miko na maadili ya chama na baadhi ya wanachama wakitaka wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wanachama wengine.