Zenj FM
Zenj FM
22 May 2025, 5:00 pm

Berema Nassor.
Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar imesema idadi ya matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa mwezi Aprili yameongezeka kwa asilimia 30.8 hadi kufikia matukio 102 kwa mwezi wa April 2025 kutoka matukio 78 kwa mwezi wa machi 2025.
Akitoa takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar kwa mwezi wa April 2025 Mtakwimu Ahmada Suleiman kutoka Divisheniya Takwimu za Jinsia na Ajira amesema wilaya ya Kati imeripotiwa kuwa matukio mengi ukilinganisha na wilaya nyengine ambapo matukio 16 sawa na asilimia 15.7 ikifuatia wilaya ya Magharib A ambapo yameripotiwa matukio 15 sawa asilimia 14.7
Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi kutoka makao makuu ya Polisi Zanzibar Mkaguzi Makame Haji Haji amesema ni wajibu wa wazazi kuwa karibu na toto wao katika kufatilia mienendo yua watoto wao ili kuweza kuondokana na vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.