Zenj FM
Zenj FM
7 May 2025, 7:43 pm

Na Mary Julius.
Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote zanzibar , Taasisi ya PharmAccess imeanza kutoa mikopo kupitia Medical Credit Fund ili kuhakikisha azma na lengo hilo linafikiwa.
Akizungumzia utoaji wa mkopo huo, Mkurugenzi wa PharmAccess, Heri Marwa, amesema wanaendelea kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya zanzibar katika kuboresha utioaji wa huduma bora kwa wananchi visiwani zanzibar kwa kutoa mikopo nafuu kupitia medical crediti fund wadau wa sekta ya afya wa serikali na binafsi.
Mkurugenzi Heri amesema Mpango huu unalenga kuwawezesha watoa huduma wa afya – hasa wa maeneo ya vijijini na mijini yenye uhitaji mkubwa – kupata rasilimali za kuboresha miundombinu, vifaa tiba, na uwezo wa utoaji huduma kwa ujumla.
Aidha amesema kwa upande wa tanzania bara mikopo hiyo imesaidia kwa asilimiak kubwa kuboresha huduma za afya za msingi na vituo 90 vimesha jiunga.
Kwa upande wake Meneja wa ushauri Medical Credit Fund kutoka PharmAccess Delfina Thomas amesema mkopo huo ni wa muda mfupi ambapo umekusudia kuwafikia watu wenye mitaji midogo wanaotoa huduma za afya kwa kutumia vituo vya afya, na maduka ya dawa.