Radio Jamii Kilosa
Radio Jamii Kilosa
8 October 2026, 17:05

YPIT Consultancies ni kampuni imekuwa ikifungua milango kwa wanafunzi kupata fursa za elimu katika nchi mbalimbali, zikiwemo India, China, Uingereza na na huwasaidia wanafunzi wanaotafuta fursa za ufadhili na scholarships kulingana na sifa na mahitaji yao.
Kampuni ya YPIT Consultancies imefanikiwa kuwawezesha zaidi ya wanafunzi 60 kwa mwaka huu kutoka Tanzania kupata nafasi za masomo katika vyuo mbalimbali nje ya nchi, ikiwemo China, India na Uingereza, hatua inayolenga kuwafungulia vijana fursa ya kupata elimu na uzoefu wa kimataifa.

Akizungumza na Redio Jamii Kilosa wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Lilian Masine kutoka Idara ya Masoko ya kampuni hiyo alisema miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana mwaka huu ni kuwawezesha wanafunzi watatu kupata nafasi za masomo nchini Uingereza na kwamba kupata nafasi za kusoma nchini humo si jambo rahisi, hivyo kampuni imekuwa ikiwasaidia wanafunzi na wazazi kupitia taratibu mbalimbali, huku ikiendelea kutoa ofa kwa wazazi na walezi wanaotamani kuwawezesha watoto wao kusoma nchini Uingereza.
Naye Mkurugenzi wa YPIT Consultancy, Shedrack Juma Masine, aliwataka wanafunzi wanaomaliza masomo yao nje ya nchi kuhakikisha wanatumia elimu na vyeti walivyovipata kwa kujenga maisha yao na kuchangamkia fursa zinazopatikana huku akisema kuwa kampuni hiyo inaendelea kuwa na fursa mbalimbali kwa wahitimu, hivyo wanafunzi hawapaswi kuishia na vyeti pekee bali wanapaswa kutafuta namna ya kutumia taaluma zao katika kujiajiri na kuajiriwa.
Kwa upande wake, mmoja wa wazazi ambao watoto wao wamepata nafasi ya kusoma nchini Uingereza, aliishukuru YPIT Consultancy kwa kusaidia kutimiza ndoto ya mtoto wake ya kupata elimu nje ya nchi na amewahamasisha wazazi na walezi wengine kutafuta taarifa sahihi na kutumia fursa zinazopatikana ili kuwawezesha watoto wao kupata elimu bora, akisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu ya mtoto ni maandalizi muhimu kwa maisha yake ya baadaye.