Radio Jamii Kilosa
Radio Jamii Kilosa
17 June 2026, 08:52

Picha ni wamiliki wa day care pamoja na waratibu wa mradi wa Kinara Totocare.
Wadau wa shirika la Kinara lililopo Mkoani Morogoro wameendelea kuwaomba wamiliki wa shule za kulelea watoto wadogo (day care) kuendelea kusajili vituo vyao ili viweze kutambulika na mamlaka husika.
Na Aloycia Mhina
Wamiliki wa vituo vya shule za kulelea watoto wadogo mchana ( day care ) Wilayani Kilosa wametakiwa kusajili vituo vyao ili kuendana na matakwa ya serikali.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mratibu wa Day care Wilaya ya Kilosa Silvester Williamu Katikaza wakati akifunga mafunzo ya Wamiliki wa Vituo vya Day care vilivyoko katika Kata ya Dumila Wilayani Kilosa.
Katikaza amewapongeza wadau wa Shirika la Kinara lililoko Morogoro kwa kuwapatia mafunzo Wamiliki hao ikiwemo kuwataka kusajili vituo ili kuendana na kasi ya Serikali.
Aidha amewataka kusajili watoto kuanzia umri wa miaka miwili hadi miaka minne kama mfumo unavyotaka wasipofanya hivyo watakuwa wanaenda kinyume na mfumo wa Serikali wa Kusajili Vituo hivyo vya Day Care .

Pichani ni William Katikata Mratibu wa shule za Daycare Wilaya ya Kilosa.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Kinara Toto Care Prisca Norbert amesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yatawafikisha mbali na kuhakikisha vituo vinasajiliwa na kuwaomba Serikali kupitia ustawi wa Jamii washirikiane kwa pamoja, ambapo Salma Simbalyana kutoka Kinara Morogoro amewataka wamiliki kutumia mitandao ya Kijamii ili kutangaza Biashara zao ili jamii wapate kuona wanachofanya.

Pichani ni Prisca Norbert Mratibu wa Kinara Totocare Mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wa Wamiliki wa Day care Bi Paulina Ikhanga na Rachel Musa Baraja kwa kuwashukuru Ustawi wa Jamii na Wadau wa Mradi Kinara Toto care shukuru kwa kupata mafunzo hayo kwani wamejifunza vitu vingi ikiwemo malezi na ulinzi wa mtoto, Lishe Bora na uzazi wa mpango.