Radio Jamii Kilosa

Maafsa ugani Kilosa sasa kuwafikia wakulima vijijini kwa haraka.

12 April 2023, 9:29 am

Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka akikibidhi pikipiki kwa Afsa Kilimo. Picha na Ally Chimela

Serikali imewakabidhi pikipiki maafisa ugani wote wilayani Kilosa ili kuondokana na adha walioyokuwa wanaipata ya usafiri na kushindwa kuwafikia wakulima wengi kwenye mashamba yao na kutatua changamoto.

“Tunaishukuru serikali kwa kuiona kwa jicho la pekee wizara yetu ya kilimo kwa kutuletea pikipiki ambazo tutazitumia kwa kuwafikia wakulima waliopo mbali na maeneo ya kijiji kwa ajili ya kuwahudumia na kuleta tija katika kilimo”.

Na Asha Madohola

Maafisa ugani wilaya ya Kilosa wameishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki ambazo zitawasadia kuwatatulia adha waliyokuwa wakiipata ya usafiri kwa kushindwa kuwafikia wakulima wengi katika utoaji wa huduma za kilimo.

Akizungumza kwa niaba ya Maafsa ugani Bi Hadija Abdallah Dibwe mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo aliishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia pikipiki hizo ambazo zitawasadia kuwatatulia kwa wakati na kuongeza kipato kwa wakulima.

Sauti ya Afsa ugani Bi Hadija Dibwe

“Ilikua wakati mwingine ni ngumu kwa maafsa ugani kuwafikia wakulima kwa wakati kutokana na jiografia iliyopo hivyo tunashukuru Mhe Rais kuiangazia wizara ya kilimo kwa kuirahisishia kiutendaji na tunaahidi kwenda kutatua changamoto za wakulima kwa wakati”. Alisema Bi Hadija

Mkuu wa usalama barabarani Kilosa Inspekta Bakari Kiseyu

Mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Kilosa Inspekta Bakari Kiseyu aliwataka maafisa ugani hao kuzitunza pikipiki hizo kwa kuzingatia usalama kwa kutokuendesha chombo chombo cha moto wakiwa wamelewa na kutakiwa kuvaa vifaa ambavyo vitawasaidia kuwakinga na kupata madhara makubwa pindi watakapopata ajali.

Sauti ya Mkuu wa usalama barabarani Inspekta Kiseyu
Kaimu Mkurugenzi Kilosa Bi Fadhia Nondo

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Fadhia Nondo aliwataka kuwa waadilifu na waanifu katika matumizi ya pikipiki hizo katika utunzaji na kuzingatia usalama wao na hatua zitachukuliwa hatua za kinidhamu kwa watakaotumia tofauti na dhamira ya Serikali.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi Kilosa Bi Fadhia
Mwenyekiti wa halmashauri Kilosa Wilfred Sumari

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa Wilfred Sumari aliwataka maafisa kilimo hao wakazitumie pikipiki hizo kwa ufasaha, ili kuongeza tija kwa wakulima katika uzalishaji ambayo itasaidia hata katika ongezeko la mapato.

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri Sumari
Mkuu wa wilaya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mkuu wa wilaya Kilosa Shaka Hamdu Shaka alisema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa pikipiki 87 kwa maafsa ugani wilaya ya Kilosa ili wakawatumikie wakulima kwa ufasaha kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanategemea kilimo kuwaainua kiuchumi.

Sauti ya mkuu wa wilaya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka