Radio Jamii Kilosa

USAID yanufaisha vijana Kilosa kilimo cha mbogamboga, matunda

23 October 2023, 11:02 am

Waendesha mradi wa Kilimo Tija wakiwa katika mojawapo wa shamba linalisimamiwa na mradi. Picha na mtandao

Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID), kupitia mradi wa Kilimo Tija wameanza kuboresha teknolojia za kisasa za kilimo nchini Tanzania sambamba na kuweka  mifumo ya kilimo pamoja na masoko ya mazao ya mbogamboga na matunda kwa kutoa elimu kwa vitendo kwa vijana.

Na Asha Rashid Madohola

Katika kuelekea msimu wa kilimo, wakulima wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wameshauriwa kuandaa mashamba kutokana na elimu wanaoyoipata kutoka kwa wataalam wa kilimo pamoja na kujiandikisha mapema kwenye pembejeo za kilimo ambayo itawasaidia kupata mbolea kwa wakati na kuwaletea tija kwenye kilimo chao.

Sauti ya Afsa Teknolojia za Kilimo

Awali akizungumza kwa njia ya simu na Redio Jamii Kilosa, Afisa Teknolojia za Kilimo katika programu ya Kilimo Tija katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa mradi wa Kilimo Tija ambao upo chini ya usimamizi wa serikali ya Marekani alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanikiwa kuwafundisha vijana wa chuo cha MATI Ilonga na wakulima kutambua mbinu bora za kilimo bora cha mazao ya mbogamboga na matunda na kutumia kilimo tija kwa ajili ya kuwanufaisha kiuchumi.

Sauti ya Afsa Teknolojia za Kilimo akizungumza

Mkuu Wa Chuo Cha Kilimo Ilonga Felix Mrisho alisema kuwa mwaka huu wameingia makubaliano na mradi wa kilimo tija unaoendeshwa na USAID wenye dhumuni la kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu kilimo tija kupitia kilimo cha bustani kunzia uaandaji wa eneo  sahihi  kwa ajili ya kilimo, utumiaji wa mbolea na umwagiliaji bora pamoja na kilimo biashara.

Sauti ya Mkuu Wa Chuo Cha Kilimo MATI Ilonga

Mmoja wa wanufaika wa mradi huo Madam Raha ambaye ndiye Mkurugenzi wa RAHA FARM aliushukuru mradi wa kilimo tija kwa kuwa umekuwa mwangaza kwa vijana wengi kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda hususan RAHA FARM ambao wanajihusisha na uzalishaji wa miche ya nyanya walipatiwa mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara.

“Mboga na matunda walinitaka kufanya kwa ajili ya kibiashara laikini nilikiona ni kigumu hata nilipowatembelea wakulima kuwaambia kutumia mbegu za kwenye trei waliona ni gharama kubwa hivyo niliona siwezi kufanya kama biashara lakini mboga na matunda walizidi kunishauri lazima nifanye kilimo biashara” alisema Madam RAHA.

Sauti ya Mkurugenzi wa RAHA FARM

Kwa upande wake Daines Mtei Mratibu kutoka Wizara ya Kilimo aliwahukuru USAID kwa kuwashika mkono serikali katika kuinyanyua sekta ya kilimo na kuwapa mafunzo bora ya kilimo na kuwafanya wakulima watumie kilimo tija kama biashara na kuwanufaisha kiuchumi na serikali ipo tayari kuwa nao begabega ili kuendeleza ufadhili huo.

Sauti ya Mratibu wizara ya kilimo

Naye Chief of Party USAID Mr Anthony  Coello alisema kuwa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), limesema muhimu kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, ili kufikia malengo ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vijana wanapatiwa mafunzo ya kilimo tija.

Sauti ya Mr Anthony