Radio Jamii Kilosa

Mlimani Boma watengeneza barabara ya zaidi ya mita 400 kupitia Tasaf

5 September 2023, 8:44 am

Barabara iliyopo kitongoji cha Mlimani Boma iliyotengenezwa na mradi wa Tasaf. Picha na Asha Madohola

Kukamilika kwa barabara hiyo kuleta neema kwa wananchi wa Mserereko ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu ili kupata usafiri wa kuwapeleka kwenye mahitaji yao ya kijamii kama huduma za afya ambapo ikitokea mgonjwa au amefariki wanambeba mikononi kurudisha nyumbani.

Na Asha Madohola

Wakazi wa kitongoji cha Mlimani Boma kilichopo kata ya Kasiki wilayani Kilosa kwa kushirikiana na Mwenyekiti wao kitongoji Hosea Nicodemas Mgunda wafanikiwa kutengeneza miundombinu ya barabara huku Serikali ikiwaunga mkono kwa kutengeneza makaravati kwa ajili ya kupitisha maji kipindi cha masika.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlimani Boma Hosea Nicodemas Mgunda akielezea mradi wa barabara

Akizungumza na Redio Jamii Kilosa iliyofika katika barabara na kuona namna shughuli za utengenezaji wa barabara ukiendelea Mwenyekiti huyo alisema anaushukuru mradi wa Tasaf pamoja na mdau wa maendeleo ambao kwa kushirikiana na wananchi wamefanikisha kukamilika kwa barabara ambapo awali hakukua na barabara.

sauti ya Mwenyekiti Mgunda akizungumzia mradi wa barabara
Mwenyekiti wa Mlimani Boma akielezea kazi inayofanyika

Aidha Mgunda alisema kwa sasa hali usafiri katika kitongoji hicho inaridhisha na wananchi sasa wanapata huduma za kijamii kwa urahisi kama usafiri na utengenezaji wa barabara hiyo upo hatua ya ufyatuaji wa makaravati huku akiishukuru serikali kwa uwezeshaji huo.

Sauti ya Mwenyekiti Mgunda akizungumza

Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi wa kitongoji hicho kuitunza barabara hiyo ili iweze kudumu kwa kuwa imekua mkombozi wa maendeleo ambapo kwa sasa wapo mbioni kutatua changamoto ya umeme na maji ili waondokane na adha ya kutumia maji ya mtoni.

Wananchi wanao wajibu wa kuitunza hii barabara haijalishi upo katika mradi wa Tasaf ama haupo na msidhani serikali itaendelea kutoa msaada kwa ajili ya hii barabara na barabara inapokuwepo ndio maendeleo yanafunguka” alisema Mgunda.

Sauti ya Mgunda

Kwa upande wake mwananchi wa ktongoji hicho aliyefahamika kwa jìna la Baby Makoko alisema anaishukuru Tasaf na serikali kwa kuwawezesha kupata barabara ambapo awali walikuwa wakikabiliwa na adha ya ukosefu wa barabara lakini kwasasa wanaiomba serikali iwapelekee huduma ya maji katika eneo lao.

Sauti ya mkazi bi Makoko