Radio Jamii Kilosa

Wakulima wa Kilosa wanashauriwa kupanda alizeti

21 April 2023, 10:42 am

Afisa kilimo kata ya Mbigiri Gerald Gabriel Njimbali. Picha na Asha Madohola

Zao la alizeti ni zao ambalo ni la muda mfupi pia linastahimili mvua kidogo hivyo mkulima atanufaika kwenye mazao ambayo atajikwamua kiuchumi kwa haraka tofauti na mazao mengine.

“Mvua zimerudi kwa kipindi kingine ambacho mkulima awali alipanda mazao kama mahindi na mpunga lakini mvua zilikua chache mazao yakakauka hivyo kwa sasa nawashauri kupanda alizeti”.

Na Asha Madohola

Wakulima wilayani Kilosa wameshauriwa kuziitumia vema mvua zilizorudi katika kipindi hiki kwa kupanda mbegu za muda mfupi ambazo zinastamili ukame.
Akizungumza Afisa kilimo wa kata ya Mbigiri Gerald Gabriel Njimbali amesema kipindi hiki cha mvua wakulima wanatakiwa kuachana na kulima zao la mpunga kwa kuwa mvua zitakapokata hautaweza kumea hivyo kwa sasa wanatakiwa kulima zao la alizeti kwa kutumia mbegu za kisasa.

Sauti ya Afisa kilimo Bw Njimbali

“Mahindi kipindi cha mvua cha kwanza mahindi yalimea vizuri sana lakini ulitokea ukame ambao uliathiri mazao yote na kwa sasa mvua zimerudi hivyo niwashauri wakulima walime mazao ya alizeti ambayo ni ya muda mfupi lakini hata mvua ikikata yanavumilia ukame”.

Mbegu ambayo wakulima washauriwa kuitumia

Bw Njimbali alisema licha ya kuwahamasisha wakulima kulima katika kipindi hiki kwa kutumia mbegu za kisasa lakini bado mpaka hawana mbegu za ruzuku, isipokuwa wanafanya kazi na makampuni ambayo huwaletea na kuwauzia kwa bei nafuu kwa wakulima waliojisajili.

Sauti ya Afisa Kilimo Njimbali akizungumzia mbegu za ruzuku

Hata hivyo Afisa kilimo huyo aliishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki ambayo imewarahisishia kuwafikia wakulima wengi na kuwapatia huduma ambayo italeta tija katika kilimo licha ya kukabiliwa na changamoto ya mafuta.

Sauti ya Afisa kilimo Bw Njimbali