Radio Jamii Kilosa

Jeshi la Polisi laongoza zoezi la usafi Kilosa

30 January 2023, 9:32 am

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilosa  (OCD)  Hasani Selengu ameliongoza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilosa Katika  Kufanya Usafi  katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa leo Januari 27 Mwaka huu 2023 ..

Wakati wakendelea kufanya  usafi huo  wa kufyeka nyasi na miti amesema wameshiriki kufanya usafi huo ikiwa ni muendelezo wa Kutimiza Dhana ya Polisi jamii kwa kuwa karibu na Jamii kushiriki katika Shughuli mbalimbali za kijamii ..

OCD Hassan Selengu pichani hapo juu akiwa na polisi Hospitali ya wilaya ya Kilosa wakifyeka nyasi.

OCD KILOSA akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi

Aidha akitoa Shukrani kwa Jeshi la Polisi mara baada ya kufanya usafi huo Kaimu Afsa  Afya na Mazingira kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kilosa Mbaraka  Lilanga amelishukuru Jeshi hilo la Polisi Wilaya ya Kilosa kwa niaba ya Mganga mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya  kwa kushiriki kufanya  usafi huo kwani litaepusha wadudu katika Maeneo hayo ya Maabara na Icu kutokana kulikua na Majani marefu kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha..

Kaimu Afsa Afya na Mazingira kutoka hospitali ya wilaya ya Kilosa akitoa shukrani

Katika hatua nyingine Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilosa Shabani Mdoe amesema wilaya ya Kilosa itakuwa na ugeni wa Ziara ya Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Godfrey Daniel Chongolo  Siku ya Jumapili Januari 29  Mwaka huu 2023.

Katibu Mkuu wa CCM wilaya ya Kilosa Shabani Mdoe akitoa taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu Taifa wilayani Kilosa