Radio Jamii Kilosa

Wadau watoa maoni habari za uongo zinavyoleta taharuki kwenye jamii

9 September 2024, 20:41

Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro Bi Joyce Nyangi. Picha na

Mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha ongezeko la upashaji wa habari zisizo na ukweli kwa sababu watu wamekuwa wakitafuta umaarufu ama ufuatiliwaji na watu wengi katika kurasa za mitandao ya kijamii kwa kuwachafua wengine jambo ambalo mamlaka inapaswa kuweka misingi thabiti ya kulidhibiti kuepuka madhara yatokanayo na kadhia hiyo.

Na Asha Madohola

Imeelezwa kuwa kuongezeka kwa umiliki wa vyombo vingi vya upashanaji wa habari na waandishi wa habari wasio kuwa na taaluma kwa kushindwa kufahamu maadili ya uandishi wa habari unasababisha kutolewa kwa habari zisizo na ukweli zimekua zikileta taharuki katika jamii na madhara kwa wahusika.

Hayo yalielezwa na baadhi ya wanawake wakati wakichagiza mada iliyoendeshwa katika kituo cha Redio Jamii Kilosa iliyokuwa ikisema namna ambavyo habari za uongo zinavyoleta athari katika jamii ambapo wamedai taarifa nyingi za uongo zinatokea katika mitandao mingi ya kijamii ambayo ndio imekua chanzo kikubwa cha utoaji wa habari za uongo.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM mkoa wa Morogoro kutokea wilayani Kilosa Bi Joyce Hamis Nyangi alisema kuwa umefika wakati muafaka serikali kuchukua hatua kwa kuweka sheria kali ambazo zitasaidia kudhibiti wimbi la waandishi wa habari wasio taaluma ambao wamekuwa wakitoa habari ambazo sio za kweli na kupelekea taharuki kwenye jamii.

Sauti ya Mjumbe Bi Joyce Nyangi
Glady’s Mapeka mwandishi wa habari mkongwe

Naye Glady’s Mapeka ambaye ni mwandishi mkongwe wa habari alisema kuwa kuna baadhi ya waandishi wamekuwa wakiandika habari bila ya kuweka usawa na huishia kutoa habari sio sahihi na kupelekea kuharibu taswira nzima ya mhusika lakini pia wasio na taaluma wamekua mwiba kwa viongozi na watu maarufu ambapo hutumika kuwachafua hivyo ameiomba mamlaka kuifanyia kazi kadhia hiyo.

Sauti ya Glady’s Mapeka

Kwa upande wake mmoja wa mdau alichangia katika mada hiyo akisema habari za uongo ama ambazo hazina ukweli zimekua zikileta taharuki kwa jamii na kwamba waandishi wengi wasiokua na taaluma wamekua hawafuati maadili na miiko ya uandishi wa habari.

Sauti ya mdau akichangia mada