Radio Jamii Kilosa

Mmomonyoko wa maadili wawaibua viongozi wa dini Kilosa

16 April 2023, 6:28 pm

Shekhe Mkuu wilayani Kilosa Alhaj Nassoro Milambo akizungumza. Picha na Yusuph Kayanda

Wananchi waaswa kuwa na karibu na watoto ili kuwafundisha maadili mema ambayo yatawasaidia kujihusisha na matendo maovu ikiwemo ushoga ambao umeikumba dunia kwa sasa.

“Dunia kwa sasa imegubikwa na ushoga vijana wengi wengi wanaingia kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni kutokana naa mmomonyoko wa maadili uliopo na kusainishwa mikataba ya siri”.

Na Asha Madohola

Viongozi wa dini ya kiislamu wilayani Kilosa wametakiwa kuungana na madhehebu mengine ili kukemea vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga) ambayo kwa sasa maaswi hayo yameikumba dunia.

Shekhe Mkuu wa wilaya Alhaj Nassoro Milambo aliyasema hayo wakati wa iftari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Aidan Kabudi katika msikiti wa kata ya Dumila na kuhudhuriwa na waislamu ambao wapo katika kumi la mwisho la kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Viongozi na waumini wakipatiwa futari

“Dunia kwa sasa imegubikwa na vitendo vya ushoga na kuna taasisi ambazo zinaletwa nchini zenye malengo ya kuwasaidia vijana lakini kuna mikataba ya siri ili waweze kusaidiwa lazima wakubaliane na mapenzi ya jinsia moja”alisema Shekhe Milambo.

Sauti ya Shekhe Nassoro Milambo
Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Kabudi

Akizungumza kwenye iftari hiyo Mbunge wa jimbo la Kilosa Mhe Prof Palamagamba Kabudi alisema elimu ya darasani na madrasa vinatakiwa viende sambamba ili kuwafundisha maadili kwa kuwasimamia kwa kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili.

Sauti Mbunge Kilosa Prof Kabudi
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka, alimshukuru Prof Kabudi kwa kuwakusanya wananchi pamoja na kuwafuturisha kutokana na upendo wake na kwamba anashirikiana vema na Rais Mhe Dokta Samia katika kuiletea maendeleo wilaya ya Kilosa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kilosa Mhe Shaka

Mhe Shaka alisema kuwa kutokana na uwakilishi mzuri wa viongozi wilayani hapa serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ambayo yatawainua kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kilosa Mhe Shaka