Radio Jamii Kilosa

Siku ya Redio yaadhimishwa Kilosa

13 February 2023, 3:57 pm

Watangazaji kipindi cha Mamo Mseto wakiwa kwenye kipindi. Picha na Salumu Juma.

Siku ya Redio duniani huadhimishwakila ifikapo Tarehe 13, Februari kila mwaka, ambapo siku hii ilianzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), mnamo mwaka 2012 mara baada ya baraza kuu la Unesco kutambua umuhimu wake. Mnamo mwaka 1946, tarehe 13 februari shirika hilo liliweza kuanzisha Redio ya Umoja wa Mataifa.

Na Epiphanus Danford

Katika kuadhimisha siku hii ya Redio duniani, Leo 13 Feb 2023 yenye kauli mbiu isemayo REDIO NA AMANI, Redio jamii Kilosa kupitia kipindi chake cha Mambo Mseto kimeweza kuzungumzia siku hii kwa kuwashirikisha wasikilizaji katika kuchangia maoni mbalimbali.

‘’Siku ya leo ni siku kubwa sana kwa Dunia na Tanzania, kwa Waandishi wa habari, Watangazaji na hata wasikilizaji pia naweza nikasema ni siku ya watu wote duniani”

Sauti za Watangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto wakizungumzia Siku ya Redio Duniani.

Aidha kwa kuangalia umuhimu wa kutumia redio katika kutoa habari ambayo inasaidia kukuza Uhuru wakujieleza na usawa wa kila kitu katika jamii na wasikilizaji wameonesha namna ambayo redio inatumika kuhabarisha na kuleta amani.

Sauti za baadhi ya wasikilizaji wakitoa maoni yao juu ya Siku ya Redio Duniani.

Nae mmoja kati ya Watangazaji wa Kituo hicho cha Redio Jamii Kilosa aliweza kuzungumzia siku ya Redio duniani kwa nafasi yake ya kipekee na aliweza kusema kuwa.

‘’Siku ya leo ni siku kubwa sana kwa Dunia kwa Tanzania, kwa Waandishi wa habari, Watangazaji na hata wasikilizaji pia naweza nikasema ni siku ya wote duniani. Kwasababu hakuna asiyeifahamu redio na hakuna asiyesikiliza redio lakini kwa kipekee nichukue nafasi hii kama mtangazaji ni siku yangu kubwa lakini ni siku yetu wote hapo ofisini.(Redioni).

Sauti ya Mtangazaji wa Redio Jamii Kilosa akizungumzia siku ya Redio duniani.