Radio Jamii Kilosa

Kilele cha wiki ya wananchi Kilosa, Yanga wafanya usafi kliniki ya mama na mtoto

23 July 2023, 11:37 am

Kutoka kulia ni Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa John Mwaluko na wa pili Katibu Mkuu Abdallah Pocho. Picha na Asha Madohola

Na Asha Madohola

Katika kusherekea kilele cha wiki ya wananchi Julai 22 wanachama na mashabiki wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika Kliniki ya Mama na Mtoto Kilosa.

Wananchi hao wa jangwani waliamua kuungana kwa pamoja ili kufanya shughuli ya kijamii yenye lengo na dhamira ya kuiombea mema na matokeo mazuri ya timu yao ya Yanga kwenye msimu mpya wa ligi kuu 2023/2024 ikiendeleza matokeo mazuri ya msimu uliopita kwa kutwaa mataji ya makombe yote yaliyowaniwa likiwemo kombe la ligi kuu Tanzania bara.

Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini Abdallah Pocho
Sauti ya Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini Abdallah Pocho akizungumza
Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa Mjini
Sauti ya Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa Mjini John Mwaluko akizungumza
Msaidizi Afisa wa Afya na Mazingira Hospitali ya wilaya ya Kilosa Mbaraka Lilanga
Msaidizi Afisa wa Afya na Mazingira Hospitali ya wilaya ya Kilosa Mbaraka Lilanga