Radio Jamii Kilosa

Mfumo wa TAUSI watambulishwa kwa wafanyabiashara Kilosa

28 March 2023, 3:23 pm

Wafanyabishara wakifuatilia mafunzo ya ukataji wa leseni. Picha na Glady Mapeka

Wafanyabiashara wilayani Kilosa kuanza kunufaika na matumizi ya mfumo wa Tausi ambao utawarahisishia upatikanaji wa leseni kwa haraka.

“Mfumo huo unaweza kutumika kupitia simu janja kwa mfanyabiashara na ili kufanikisha kutumia mfumo huo mfanyabiashara atatakiwa kuwa na namba ya NIDA yenye majina ya mfanyabiashara husika, TIN namba, namba ya simu ambayo imesajiliwa” alisema Jukulu.

Na Gladys Mapeka

Elimu ya mfumo Tausi wa kukata leseni za biashara na kufanya malipo ,kukata vibali mbalimbali na kutoa kodi za Serikali bila kufika katika ofisi husika za halmashauri umeanza rasmi kutolewa kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Akitoa Elimu hiyo Afisa Biashara Wilaya Idrisa Jukulu kwa wafanyabiashara wa Tarafa ya kimamba na Kilosa amesema mfumo huu ni mfumo mpya uliotolewa na TAMISEMI utawarahisishia wafanyabiashara wote na wanaolipa ushuru mbalimbali kufanya malipo na kukata lesen sehemu yoyote walipo bila kufika ofisi za Halmashauri kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Afisa Biashara wilaya Idrisa Jukulu pichani kushoto akitoa elimu ya mfumo wa Tausi

Aidha alifafanua kuwa mfumo huo utaanza kutumika rasmi kuanzia mwezi wa saba mwaka huu, kwasasa umeanza kutumika kwa wateja wapya ambao wanafungua biashara zao ambazo zinahitaji lesen za biashara .

” Mfumo huu unaweza kutumika kupitia simu janja kwa mfanyabiashara ambapo ili kufanikisha kutumia mfumo huo na taratibu nyinginezo mfanyabiashara atatakiwa kuwa na namba ya NIDA yenye majina ya mfanyabiashara husika, TIN namba, namba ya simu ambayo imesajiliwa” alisema Jukulu

Hata hivyo amesisitiza kuwa mfanyabiashara atakayeomba leseni ya biashara kwa njia ya mfumo wa Tausi anatakiwa kuchagua aina ya leseni ya biashara anayoifanya na kwamba kinyume na hapo ni kosa kuomba leseni tofauti na biashara unayoifanya na kwamba mfanyabiashara yoyote atakayekiuka taratibu hizo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.