Radio Jamii Kilosa

Wanawake Kilosa watakiwa kuchangamkia fursa za uongozi

23 February 2024, 6:43 pm

Mwenyekiti wa UWT Kilosa Bi Jamillah Miyonga akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM. Picha na Yunus

Uchaguzi wa serikali za mitaa\vitongoji na vijiji utakafanyika mwaka huu 2024 ili kuchagua viongozi katika nafasi hizo ambazo zitawapa fursa ya kwenda kuwaongoza wananchi katika kuwaletea maendeleo kwa kuzingatia sheria na miongozo.

Na Asha Madohola

Wanawake wametakiwa kuchangamkia fursa kipindi cha uchaguzi serikali za mitaa/vijiji kwa kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili washirikiane kuleta maendeleo wilayani Kilosa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilosa ndugu Jamillah Miyonga leo 23 Februari 2024 katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kilosa iliyofanyika ukumbi wa Mamboya uliopo wilayani hapa.

Aidha, Bi Miyonga amesema pia kuwa watashirikiana vyema na makatibu ili kuangalia nafasi zilizopo wazi ili watoe nafasi kwa wanawake kuingia ngazi ya kugombea wanawake katika uchaguzi wa vitongoji na vijiji.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilosa akizungumza

“Nitafurahi kuona katika vijiji 138 kuona vijiji 50 vikichukuliwa na wananchi ambao ni wenyeviti na makatibu wa UWT” alisema Mwenyekiti wa UWT Bi Miyonga.

Sauti ya Mwenyekii wa UWT wilaya ya Kilosa ndg Jamillah Miyonga akizungumza

Hata hivyo alisema kuwa wanawake ndio wenye ushawishi kwenye jamii na kwamba katika vitongoji 814 ataweka mikakati ya ndani ya wanawake kuzoa vitongoji zaidi ya 300.

Madiwani, wenyeviti na makatibu wakifuatilia mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM