Radio Jamii Kilosa

Abaka na kulawiti wadogo zake wawili Kilosa

21 February 2023, 2:21 pm

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi ”B” Ndugu Halfani Likungulu .Picha na Beatrice Majaliwa

Vitendo vya kikatili vinavyoendelea dhidi ya Watoto wadogo bado ni tatizo kubwa katika jamii zetu tunazoishi,hali inayopelekea watoto kukatisha ndoto zao kutokana na ukatili wanaofanyiwa.

Na Beatrice Majaliwa

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilosa linamshikilia George Idd (19) mkazi wa kitongoji cha Mbumi B kata ya Mbumi Wilayani Kilosa kwa tuhuma za kubaka na kulawiti  watoto wawili wa kike mwenye umri wa miaka 6 na mwingine 8 ambao wote ni ndugu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi B Halfani Likungulu amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kutokana na ukatili waliofanyiwa watoto hao na kwamba mtuhumiwa amefikishwa kituo  cha polisi kwa uchunguzi na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi ”B” ndugu Halfani Likungulu.

Likungulu amesema kuwa tukio hilo limefahamika nyumbani kwao majira ya usiku baada ya mgeni aliyelala na watoto hao kushuhudia kijana huyo akimuingilia kimwili mmoja wa watoto hao katika kitanda walichokuwa wamelala.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi ”B” ndugu Halfani Likungulu.

“Baada ya mahojiano huyu kijana ameanza kukifanya muda mrefu na huyu mtoto wa miaka sita ni ndugu yake wa baba mmoja na mama mmoja na amekuwa akiwa akiwabaka na kuwalawiti ndoma vitendo vya kikatili vinavyoendelea dhidi ya watoto bado ni kubwa katika jamii zetu tunazoishi hali inayochangia kukatisha ndoto zao kutokana na ukatili wanaofanyiwa”alisema Mwenyekiti huyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi ”B” ndugu Halfani Likungulu.

Akizungumza mmoja wapo wa wazazi wa watoto hao Suzana Kidego (siyo jina lake halisi) amesema kuwa alianza kusikia harufu mbaya kutoka kwa watoto hao lakini hakujua kama watoto hao wameingiliwa kimwili hali.

Sauti ya Mzazi mmoja wapo wa watoto hao akizungumzia namna tukio lilivyo tokea.

Mmoja wa watoto hao Juliet Mussa (06) (siyo jina halisi ) amesema kuwa mtuhumiwa alianza kuwaingilia kimwili siku nyingi za nyuma na walishindwa kutoa taarifa kwa wazazi wao kutokana na kutishiwa vitisho ikiwemo kipigo.

Sauti ya mtoto aliyefanyiwa kitendo cha kikatili.

Kwa upande wake jirani wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina na mama Mungi amesema kuwa watoto hao walikatazwa kucheza na wenzao ili wasije wakatoa taarifa hizo kwa watu.

Sauti ya mmoja wa majirani anayefahamika kwa jina la Mama Mungi akizungumzia tukio lilivyotokea.