Radio Jamii Kilosa

Watumishi wapya watakiwa kuitumikia jamii kwa kuzingatia uadilifu

6 July 2023, 7:04 am

Watumishi wapya wakifuatilia semina elekezi ya utendaji kazi. Picha na Gladys Mapeka

Watumishi wapya kutoka Idara za Afya ,Elimu msingi na sekondari wametakiwa kujua kuwa wana jukumu la kutumikia jamii pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii ya Kilosa.

Na Gladys Mapeka

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Ndg Kisena Mabuba

Akizungumza na watumishi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg.Kisena Mabuba alisema kuwa wanapaswa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma sambamba na kufanya shughuli za kuwapatia kipato halali jambo litakalowasaidia kutunza ajira zao.

Afisa Utumishi na Utawala Bi Fauzia Nombo

Kwa upande wake Afisa Utumishi na Utawala Bi. Fauzia Nombo aliwataka watumishi hao kuuzingatia wajibu wao kwa kuhakikisha wanafuata sheria,kanuni na taratibu za kiutumishi.

Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi Bi Zakia Fandey

Hata hivyo Mkuu wa Divisheni ya elimu Sekondari Joseph Kapere na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi bi Zakia Fandey waliwataka watumishi hao kufahamu mifumo mbalimbali iliyotolewa na Serikali kwaajili ya utendaji kazi sambamba na kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa Miradi ya maendeleo ili kuleta tija kwani Serikali imewaamini na kuwategemea.