Radio Jamii Kilosa

Soya imefungua fursa Kilosa

15 September 2026, 13:28

Afisa Kilimo wilaya ya Kilosa Elina Danstan akitoa elimu kuhusu zao la soya. Picha na Stamius Kyombo

Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye umuhimu mkubwa katika chakula na uchumi ambapo inaelezwa kuwa kwa kutumia mbegu bora, kanuni sahihi za kilimo na teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji na tija.

Na Beatrice Majaliwa

Wakulima wa zao la soya wametakiwa kuendelea kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya soko na kuongeza kipato kwa wananchi.

Wito huo ulitolewa na mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mkulima yaliyofanyika katika kata ya Msowero Afisa kilimo Wilaya ya Kilosa Elina Danstan aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambapo alisisitiza umuhimu wa wakulima kutumia fursa zilizopo katika kilimo cha soya.

Bi Elina alsema kuwa zao la soya lina umuhimu mkubwa kutokana na matumizi yake katika sekta mbalimbali, hivyo wakulima wanapaswa kuongeza juhudi katika uzalishaji kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na amewataka wakulima kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha elimu kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa kilimo cha soya.

Sauti ya Afisa Kilimo Elina Danstan

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Resilient Soy for Empowerment in Tanzania (RESET) Hussein Aire alisema mradi huo umekuwa na mafanikio mbalimbali kama vile kuwafikia na kuwajengea uwezo wakulima kupitia mafunzo na kupia uanzishaji wa mashamba ya darasa na mashamba ya uzalishaji.

Sauti ya Mratibu RESET Hussein Aire

Sambamba na hayo mmoja kati ya wakulima na mnufaika wa mradi huo Pili Mwangoka kutokea katika kijiji cha Peapea alisema kuwa kupitia zao hilo ameongeza mnyororo wa thamani kwa kupata bidhaa mbalimbali zinazotokana na soya.

Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea mafunzo kuhusu kilimo cha soya
Sauti ya mkulima Pili Mwangoka

Maadhimisho hayo ambayo yaliandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa kushirikiana na wadau wa mazingira Taasisi ya Danida Green Business Partnerships (DGBP) ambapo wakulima wa zao la Soya walikutanishwa na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha, wanunuzi, watafiti pamoja na wasimamizi wa sekta ya kilimo na kupata nafasi ya kujengewa uwezo juu ya uzalishaji, fursa za masoko na mitaji.