Radio Jamii Kilosa

Watumishi wa umma wapatiwa mafunzo

14 September 2026, 11:54

Afisa Ustawi wa Wilaya ya Kilosa John Mpogole. Picha na Stamius Kyombo

Watumishi hao wameaswa kuzingatia sheria kanuni na miongozo ya kiutumishi

Na Ally Ibrahim

Watumishi wa umma na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya ya Kilosa wamepatiwa mafunzo ya Uongozi wa mguso juu ya kutambua masuala ya ukatili wa kijinsia na athari zake na namna ya kudhibiti katika jamii ili kulinda usalama wa mtoto na watoto wilayani humo.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo Afisa Ustawi wa jamii na masuala ya ukatili wa kijinsia John Petro Mpogole alieleza matarajio yake baada ya mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuona mabadiliko kutoka kwa viongozi na watu wote walioshiriki mafunzo hayo.

Sauti ya Afisa Ustawi wa jamii John Mpogole
Mwezeshaji kutoka Uzikwasa Nickson Lutende

Aidha mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo ya mguso kutoka taasisi isiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na serikali UZIKWASA Nickson Lutende alisema lengo la kufanya mafunzo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni kuleta mabadiliko juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na jamii kwa ujumla kupitia viongozi wakiwa nyumbani, kazini au mtaani.

Sauti ya mwezeshaji kutoka Uzikwasa Nickson Lutende

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo Shulule Expedito Ngadaya ambaye ni Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu wilaya ya kilosa alisema manufaa aliyoyapata kwenye mafunzo hayo yatamfanya kuwa balozi juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Shulule Expedito