Radio Jamii Kilosa

Maafisa maendeleo waaswa kuwa wabunifu

2 September 2026, 12:29

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Morogoro Bwana Gibson Mwakoba (katikati) akizungumza na maafisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kilosa. Picha na Epiphanus Danford

Maafisa hao waaswa kutumia fursa

Na Aloycia Mhina

Maafisa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wametakiwa kuwa wabunifi na kutumia taaluma zao kutafuta njia mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 1, 2026 na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Morogoro Gibson Mwakoba wakatika akizungumza na maafisa maendeleo wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa lengo likiwa kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji wao kazi.

Mwakoba amesema kuwa Maafisa maendeleo wanapaswa kuhamasisha wananchi kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi, vikundi vya uzalishaji na miradi ya maendeleo.

Picha ni Maafisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Ameongeza kuwa wataalamu hao kutumia ubunifu na teknolojia katika utoaji huduma ,pamoja na kuhakikisha fursa mbalimbali za Serikali zinawafikia wananchi kwa wakati, ambapo hatua hiyo inaongeza ufanisi katika huduma za maendeleo na kuhakikisha kutoa taarifa za vikundi vilivyokosa mikopo ni sababu gani zimepelekea vikundi hivyo kukosa mikopo lengo likiwa wakati mwingine wawe na vigezo vinavyokidhi uombaji mikopo.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Morogoro Bwana Gibson Mwakoba akizungumza na maafisa maendeleo ya jamii wilaya ya Kilosa.

Picha ni Maafisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Aidha Mwakoba amewataka Maafisa hao kutoa Elimu kuimarisha familia za wananchi kama msingi wa maisha kwa kuwatembelea ,wasisubirie mikutano wanapaswa wazijue familia katika kata zao ikiwemo kutumia rasilimali walizo nanzo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Dedani Maube aliyekuwa amemkaimu Afisa maendeleo ya Wilaya ya Kilosa katika Kikao hicho, amewataka kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyoelezwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Kilosa Bwana Dedani Maube.

Picha ni Dedani Maube afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.