Keifo FM
Keifo FM
30 May 2025, 15:53

Wandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wamekumbushwa kuzingatia misingi na weledi katika kuandika habari zenye tija na kuziweka kwenye mtandao wa radio portal ili kuwafikia wasikilizaji nje ya mikoa yao
Na Emmanuel Jotham
Wandishi wa Habari wa Radio wametakiwa kutumia jukwa mbalimbali za miandao ili kufikisha habari zao nje ya mipaka ya Radio zao ili kuwafikia walengwa wa habari hizo walio nje ya maeneo yao kufikisha habari.
Akizungumza na Wana habari katika Mafunzo yaliyo andaliwa na Tanzania Development Information organization (TADIO) Mkoani mbeya ulio jumuisha Radio 12 na wanahabari 24 kutoka Mikoa mbalimbali FATMA ALLY kutoka TADIO amesema Mtandao una maana kubwa katika kuhakikisha habari zinafika kwa hadhira iliyo kusudiwa.
Bi Fatma ally amesema kuwa kwa sasa Radio Portal inayo endeshwa na Tadio ina makusudi makubwa ya kuhakikisha tunatanua wigo wa kuwafikia wasikilizaji walio nje ya mikoa yetu.
Sara Musiba ni miongoni mwa wana habari walio shiriki mafunzo hayo kwa niaba ya washiriki amesema kuwa Radio Portal inayo endeshwa na Tadio imekuwa na msaada mkubwa katika kuwafikia wasikilizaji walio nje ya mkoa na nchi ya Tanzania kwa ujumla.
Aidha Radio Portal imekuwa na msaada mkubwa katika swala la masoko kwa sababu pia mtandao huo wa Radio Tadio unatoa fursa wa Radio Kwenda mubashara kwa kutumia internet na kufika sehemu ambako Radio haifiki.

Keifo fm pia inapatikana kwenye Mtandao huo kupitia
www.radioportal/keifofm.co.tz