Karagwe FM

Recent posts

23 April 2024, 9:23 pm

Askofu Bagonza ataja kundi la wabakaji Karagwe

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Mch.Dk Benson Bagonza. Picha na Eliud Henry Kumekuwa na wimbi kubwa la vitendo vya ubakaji wa watoto wilayani Karagwe mkoani Kagera ambapo ndani ya kipindi kifupi kwa mujibu…

23 April 2024, 1:53 pm

Maadhimisho miaka 60 ya Muungano yaanza Missenyi

Mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamisi Mayamba Maiga (aliyevaa suti meza kuu) Picha na Respicius John Shamrashamra za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimeanza rasmi kote nchini kwa namna tofauti ambapo baadhi ya maeneo…

22 April 2024, 5:00 pm

Madiwani Missenyi walalamikia kasi ndogo ujenzi wa VETA

Baadhi ya madiwani (kamati ya fedha, uchumi na mipango) halmashauri ya Missenyi wakiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo John Paul Wanga (mwenye notebook na karatasi kulia). Picha na Respicius John Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani…

22 April 2024, 8:43 am

Wananchi wapewa mbinu za kukomesha uhalifu

Jamii bila uhalifu inawezekana ikiwa ushirikiano na utoaji wa taarifa kwa wakati kwa jeshi la polisi vitapewa kipaumbele. Na Eliud Henry: Wananchi wilayani Karagwe wametakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuripoti vitendo vya kihalifu  ili kudumisha amani katika…

21 April 2024, 5:21 pm

CCM Kagera: Rweikiza ametekeleza ilani kwa kishindo

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazir Karamagi. Picha na Abdullatif Yunus Chama chochote cha siasa huandaa ilani kama dira ya kutekeleza vipaumbele vya mahitaji ya wapiga kura pindi kinaposhika dola baada ya uchaguzi mkuu wa viongozi.Chama cha mapinduzi CCM…

20 April 2024, 9:30 pm

TCRA yawaasa wafanyakazi Karagwe FM kuongeza ubunifu

Meneja wa mamlaka ya mawasiliano Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salumu Banali (aliyesimama) akiongea na wafanyakazi wa Radio Karagwe. Picha na Eliud Henry Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano umeendelea kwa kasi ya hali ya juu na kusukuma juhudi…

20 April 2024, 1:59 pm

Serikali kujenga mabweni mawili sekondari Bugene

Shule ya sekondari Bugene wilayani Karagwe. Picha Na. Eliud Rwechungura Licha ya jitihada kubwa za serikali kuboresha miundo mbinu, shule nyingi za msingi na sekondari za umma hukabiliwa na baadhi ya changamoto ambazo kila mara huziwasilisha kwa viongozi wanapopata fursa…

19 April 2024, 2:39 pm

Bashungwa akunwa na uwekezaji wa KARADEA

Elimu ni urithi pekee usio hamishika kwa mwanadamu, tuwapeleke watoto shule ili wapate maarifa. Na Devid Geofrey: Waziri wa Ujenzi na mbunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa viongozi na wasimamizi wa shule za serikali na binafsi…

16 April 2024, 8:10 am

DAS Karagwe akabidhi misaada ya Rais Samia kwa makundi maalum

Imekuwa desturi ya viongozi wakuu  wa serikali na mashirika ya umma na binafsi kutoa zawadi za sikukuu za kidini kama Krismas, Mwaka  mpya, Pasaka na hata Eid El fitri na eid el addha kwa ajili ya kuwezesha makundi maalum kufurahia…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171