Karagwe FM
Karagwe FM
29 May 2024, 6:05 pm
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa yenye vivutio vya utalii ambavyo havijajulikana kutokana na mkoa huu kuwa pembezoni. Chanzo cha maji moto Mutagata kilichopo katika kijiji cha Rwabigaga kata ya Kamuli kimekuwa kivutio cha utalii kwa wakazi wa mkoa…
11 May 2024, 5:51 pm
Mara nyingi viongozi kushindwa kuelewana hali inayosababisha kuchelewesha miradi ya maendeleo ya wananchi hasa upande wa uamuzi wa wapi mradi ujengwe jambo linalowaumiza wananchi wa chini wanaosubiri kunufaika na mradi husika. Na Ospicia Didace. Katibu wa chama cha mapinduzi CCM…
10 May 2024, 8:08 pm
Suala la magendo ya kahawa mkoani Kagera limekuwa suala mtambuka kila inapofika nyakati za uvunaji wa zao hilo ambapo wakulima wengi wanadaiwa kuuza maua au kuvuna kahawa mbichi na kuuza kwa njia ya magendo hasa wakulima wanaopakana na nchi ya…
10 May 2024, 10:50 am
Mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe Dkt Agnes Mwaifuge (katikati) akisisitiza jambo. Picha na Ospicia Didace. Pamoja na mkoa wa Kagera kuwa na wingi wa vyakula, ni mmoja kati ya mikoa inayotajwa kuwa na utapiamlo pamoja na udumavu kutoka na…
8 May 2024, 9:37 pm
Kampeni kabambe kwa sasa hapa nchini ni ulinzi wa mazingira kwa kudhibiti ama kupunguza matumizi ya nishati chafu yaani kuni na mkaa. Afisa maliasili na mazingira wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera bw. Rajab Kassim akishirikiana na mashirika yasiyo ya…
8 May 2024, 12:29 pm
Kumekuwa na tatizo la kuvuna na kuuza kahawa mbichi maarufu kama “Obutura “katika wilaya zinazolima zao hilo mkoani Kagera ikiwemo Karagwe. Hali hii inadaiwa kuwapunja wakulima kwani wanajikuta wakipata hasara kutokana na mauzo ya zao hilo kabla ya wakati wake.…
5 May 2024, 5:42 pm
Wako baadhi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu na wengine hupata ulemavu wanapokuwa wakubwa hivyo jamii haina budi kushirikiana kuwasaidia ili waweze kujikimu katika maisha. Na Eliud Henry: Kiasi cha Fedha sh. Mil 20 zimetolewa na shirika la kuwahudumia watu…
5 May 2024, 4:48 pm
Kitongoji Bweyaja kina tatizo la ukosefu wa maji.Wakaazi wengi wa maeneo hayo hulazimika kununua maji kwa bei ghali na hali hii inaendelea mpaka leo. Na Devid Geofrey: Wananchi wa kitongoji cha Bweyaja kijiji cha Omurulama kata ya Chanika wilaya ya…
1 May 2024, 8:40 pm
Nchi sita kati ya kumi zenye idadi kubwa kabisa ya watu kujiua duniani ziko Afrika, na kiwango cha kujiua katika bara hilo ni zaidi ya moja ya tano ikilinganishwa na maeneo mengine, WHO imesema wiki hii. Na Devid Geofrey: Mtu…
29 April 2024, 9:39 pm
Haikuwa rahisi kwa vijana wa kike kupenya na kufaulu vizuri katika taaluma kama walivyo vijana wa kiume hapa nchini Tanzania na watu wengi waliamini hivyo huko nyuma. Jambo hili pia lilisababisha wanafunzi wa kike kusita kuchagua kusoma masomo ya sayansi.…
UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.
DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.
MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.
MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171