Karagwe FM

Recent posts

4 July 2023, 11:38 am

Jela miaka 30 kwa ubakaji wa mtoto

Mahakama ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mahmoud Idi (54) mkulima mkazi wa kijiji cha Kigarama kata ya Kanyigo wilayani humo kwa kuthibitika pasipo na shaka kuwa alimbaka mtoto wa miaka minane kijijini hapo…

4 July 2023, 11:18 am

Karagwe: DC aridhishwa utekelezaji wa miradi ya elimu

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser akiwa katika shule ya msingi Kambarage iliyopata fedha za mradi wa boost: Picha na Eliud Henry Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa chini…

3 July 2023, 12:44 pm

Karagwe: Wanaodaiwa kununua ardhi kinyemela watakiwa kuwasilisha nyaraka kwa DC

Serikali wilayani Karagwe imetoa siku saba kwa wananchi walionunua ardhi ya kijiji cha Kahanga kata ya Nyakasimbi wilayani humo  kinyume cha sheria kuwasilisha vielelezo vitakavyowezesha kubaini wahusika waliowauzia  ardhi hiyo. Na Eliud Henry Wakizungumuza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na…

2 June 2023, 10:32 pm

Katibu CCM Karagwe: Leeni watoto kimaadili

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Karagwe Bw. Anathory Nshange amewataka wazazi na walezi kulea watoto wao katika maadili ya kitanzania na kiimani Bw. Nshange ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mahafali ya tano ya chuo cha Karaduce wilayani Karagwe…

2 June 2023, 10:17 pm

Homa ya marburg Kagera yatokomezwa

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameutangazia ulimwengu kuwa Kagera na Tanzania ni salama dhidi ya ugonjwa wa marburg na kwamba hakuna tena ugonjwa huo. Pamoja na hayo waziri Ummy pia amewashukuru watumishi wa wizara ya afya pamoja na mashirika ya…

28 September 2022, 6:53 pm

Fursa kibao za ajira zatangazwa kwaajili ya Wananchi

Wananchi wilayani Karagwe wamehimizwa kujiandaa ili waweze kunufaika kiuchumi kupitia Ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru utakao kesha katika uwanja wa changarawe Kayanga October 08 mwaka huu. Ni wito uliotolewa na mkuu wa wilaya Karagwe Mwalimu Julieth Binyura Sept…

2 August 2022, 3:08 pm

Makarani na Wasimamizi 409 wa Sensa Wapigwa msasa

Jumla ya watu 409 waliopita kwenye usaili wa kusimamia zoezi la sensa ambao ni makarani,wasimamizi wa maudhui na TEHAMA wameanza kupigwa msasa kwa kupewa mafunzo juu ya ukusanyaji sahihi wa takwimu za watu na makazi wakati wa sensa itakayofanyika tarehe…

11 March 2022, 8:55 am

Wakuu wa Idara wakalia kuti kavu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro kuwachukulia hatua  za kiutumishi wakuu wa Idara wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero waliohusika na ukiukwaji wa…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171