Karagwe FM

Recent posts

15 September 2023, 12:22 pm

Askofu Rweyongeza aongoza maelfu ya Mahujaji Karagwe

Kila tarehe 14 septemba waumini wa Kanisa katholiki jimbo la Kayanga wanakutana katika kituo cha hija Kalvario Kayungu kwa lengo la kusali njia ya msalaba ili kukumbuka mateso ya yesu aliyoyapata msalabani ili kuwakomboa wanadamu. Na Eliud Henry Askofu wa…

11 September 2023, 9:58 pm

Wazee wanolewa kuhusu matumizi bora ya fedha

Wazee wa kikundi cha wazee Bikolweengozi kata ya Bugandika wilayani Missenyi wameanzisha chama cha kuweka akiba ya fedha na kukopa kwa lengo la kujiinua kiuchumi. Na: Jovinus Ezekiel Missenyi Mwenyekiti wa kikundi cha wazee Bikolweengozi cha kata ya Bugandika wilayani…

11 September 2023, 12:11 pm

Zaidi ya watoto elfu 99 kupata chanjo ya polio Karagwe

Watoto 99,159 wilayani Karagwe watakuwa miongoni mwa watoto 3,250,598 wenye umri wa chini ya miaka minane watakaopata chanjo ya kinga ya polio katika kampeni ya chanjo kitaifa Septemba 21-24 mwaka huu. Na. Tumaini Anatory Kwa mujibu wa mratibu wa chanjo…

10 September 2023, 8:53 pm

Wazee watakiwa kuchangamkia bima ya afya

Na. Jovinus Ezekiel Missenyi Wazee katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kujiunga na bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma za matibabu. Akiongea   na wazee wa  kikundi cha  wazee Bikolw’engonzi kilichopo katika…

4 September 2023, 1:02 pm

Padre atoa msaada kwa watoto wenye uhitaji

Na Ospicia Didace Karagwe Mkurugenzi wa idara ya mashirika ya kipapa ya kimisionari ametoa msaada wa vyakula, nguo na vifaa vya kujifunzia vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu kwa wanafunzi wa shule msingi Mwoleka Mseto iliyoko Chabalisa katika…

6 July 2023, 8:51 pm

Wananchi Karagwe wamshukuru Rais Dkt. Samia kwa miradi ya maendeleo

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Na Ospicia Ddace Wananchi wa wilaya Karagwe wameishukuru na kuipongeza serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa…

4 July 2023, 1:04 pm

28 wapigwa msasa kwa ajili ya Uokoaji

Jumla ya Askari 28 wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali Nchini Tanzania wameshiriki mafunzo ya pamoja ili kujiongezea ujuzi utakaowasaidia wakati wa uokoaji yanapotokea majanga. Akifungua mafunzo hayo Nov 21 mwaka huu,Kamishina msaidizi mwandamizi Zabrune Levson Muhumha,Kamanda…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171