Karagwe FM

DC Maiga ahamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kwa wote

3 March 2026, 8:11 pm

Mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera Kanali mstaafu Hamis Maiga. Picha na Respicius John

Wilaya ya Missenyi imekabidhi kadi za bima ya afya kwa wote kwa makundi maalum yaliyoandikishwa kupata bima hiyo bila malipo

Na Respicius John, Missenyi

Mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamis Mayamba Maiga amezindua rasmi zoezi la usajili na ugawaji wa vitambulisho vya bima ya afya kwa wote kwa makundi maalum huku akitoa wito kwa wananchi kujiunga kwa wingi na bima hiyo ili kupata matibabu kwa gharama nafuu

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua usajili na ugawaji wa vitambulisho vya bima ya afya kwa wote kwa makundi maalum waliopata bima hiyo bure amewataka wananchi kuchangamkia bima hiyo inayotolewa kwa shilingi 150,000/= kwa kaya ya watu sita

Mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera Kanali mstaafu Hamis Maiga
Baadhi ya wananchi walioshiriki hafla ya uzinduzi wa zoezi la usajili wa wananchi kupata bima ya afya kwa wote. Picha na Respicius John

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Missenyi Dk. Jamil Yahya amesema kuwa serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuwezesha makundi maalum kupata bima ya afya kwa wote bila malipo

kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Missenyi Dk. Jamil Yahya
Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Missenyi Dk. Jamil Yahya. Picha na Respicius John