Karagwe FM
Karagwe FM
3 December 2025, 12:57 am

Halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera imepata mwenyekiti mpya Bw. Longino Rwenduru baada ya kupigiwa kura 32 za ndiyo kati ya kura 32 zilizopigwa na madiwani wa halmashauri hiyo akirithi mikoba ya mwenyekiti wa muda mrefu Wallace Mashanda aliyeenguliwa na kamati kuu ya Chama cha mapinduzi CCM Taifa katika mchakato wa awali
Na Ester Albert, Karagwe
Diwani wa kata ya Chanika ameshinda kwa kura 32 za ndiyo kuwa mwenyekiti wa hamashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera baada ya kupigiwa kura za ndiyo na madiwani wa halmashauri hiyo kutokana na kupitishwa akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Shandala baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake Desemba 2, 2025 katika ukumbi wa Angaza mjini Kayanga wilayani Karagwe bw. Longino na makamu wake wamechaguliwa kwa kura zote za madiwani wa halmashauri hiyo

Mgeni rasmi katika uchaguzi huo mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amewataka viongozi hao kutambua kuwa wamepewa wajibu mkubwa wa kuwatumikia wananchi na si vyeo vya sifa huku mbunge wa jimbo la Karagwe Innicent Bashungwa akiwataka madiwani kufuatilia miradi viporo ili kuondoa kero za wananchi hasa wasio na umeme
