Karagwe FM
Karagwe FM
3 December 2025, 12:18 am

Juhudi za kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na unyanyapaa zimeendelea kukumbwa na changamoto ya mwitikio mdogo wa wananchi kupima afya zao na matumizi hafifu ya dawa kinga kwa wanaokutwa na maambukizi
Na Ester Albert, Karagwe
Jamii wilayani Karagwe imetakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara sambamba na kuepuka ukatili na unyanyapaa kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yanayofanyika kila Desemba 1 ya kila mwaka kwa lengo la kuikumbusha jamii kuhusu kinga dhidi ya janga hilo yaliypfanyika katika kata ya Ihanda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera yametumika kwa kuijulisha jamii juu ya mapambano ya UKIMWI yanayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho yaliyobeba kauli mbiu ya “Imarisha mwitikio, Tokomeza UKIMWI” afisa maendeleo ya jamii wa kata ya Ihanda Bi Mwajuma Hamis amesema kuwa watu 521 kati ya 70,707 walipimwa na kubaini 0.7% ya waathirika

Mgeni rasmi Henriether William ambaye ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wilaya ya Karagwe kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Karagwe ameitaka jamii kuacha unyanyapaa kwa waathirika kwa kuwa kufanya hivyo kunafifisha juhudi za serikali za kupambana na janga hilo sambamba na kuwafanya baadhi ya waathirika wakimbie maeneo yao ili kujificha kwa wasiowafahamu
