Karagwe FM

Mgombea udiwani ACT Wazalendo ashusha ahadi nzito Mabale Missenyi

22 October 2025, 9:31 pm

Mgombea udiwani kata ya Mabale jimbo la Missenyi mkoani Kagera kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Mhandisi Sweetbert Kaizilege John. Picha na Theophilida Felician

Baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za kisiasa mkoani Kagera wameendelea na kampeni zao kwa ajili ya kunadi sera zao katika wiki hii ya lala salama

Na Theophilida Felician, Missenyi

Zikiwa zimesalia siku chache wananchi kutimiza haki na wajibu wao wa kuwachagua viongozi wa udiwani, wabunge na Rais, mgombea udiwani kata ya Mabale jimbo la Missenyi mkoani Kagera kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Mhandisi Sweetbert Kaizilege John ameendelea kuwafikia wananchi kitongoji kwa kitongoji akiwaeleza ahadi mbalimbali atakazozitekeleza baada ya kuchaguliwa.

Mgombea Sweetbert akiwahutubia wananchi wa kitongoji cha Kigarama kijiji Nyankele amevitaja vipaumbele muhimu vinavyomsumbua kichwa ni mapoja na suala la maji, barabara, elimu na afya ambapo uhaba wa maji imebainika kuwa nichangamoto kubwa kwa wananchi wakata hiyo.

Mbali na hayo amewahakikishia wananchi kuwa dhamira yake ni kuiona Mabale inabadilika na kupiga hatua mbele kimaendeleo kuliko ilivyo kwa sasa.

Mgombea udiwani kata ya Mabale jimbo la Missenyi mkoani Kagera kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Mhandisi Sweetbert Kaizilege John
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mabale wakimsikiliza mgombea udiwani bw. Sweetbert John. Picha na Theophilida Felician

Mikutano ya kampeni za mgombea huyo imejikita kuwafikia wananchi moja kwa moja na imeendelea kuwavutia wananchi walio wengi kutokana na ahadi zake zenye maendeleo ya kumgusa kila mmoja huku wakifurahishwa na mfumo anaoutumia katika mikutano hiyo wa kuwatengea nafasi ya kuwasikiliza changamoto na kero zao.

Katibu wa CHADEMA jimbo la Missenyi Lauriani Kabakama. Picha na Theophilida Felician

Naye katibu wa chama jimbo la Missenyi, Laurian Kabakama akiwa bega kwa bega na wagombea udiwani kata za Mabale, Kilimilile, Kyaka na Bugandika amewahakikishia wananchi wa Kigarama kuwa chama hakijakosea kuwateua wagombea hao akiwemo Sweetbert Kaizilege John hivyo wananchi wasifanye makosa yakutokuwachagua ili wayashuhudie mabadiliko makubwa ya maendeleo chini ya ACT Wazalendo

Katibu wa CHADEMA jimbo la Missenyi Lauriani Kabakama.