Karagwe FM
Karagwe FM
13 October 2025, 11:38 am

Wananchi wa kata ya Kyaka wilayani Misseyi mkoa wa Kagera wametakiwa kudumisha amani ili kulisaidia jeshi la polisi kulinda raia na mali zao hasa wakati huu taifa linapojiandaa na uchaguzi mkuu
Na Theophilida Felician Kagera.
Chama cha ACT WAZALENDO jimbo la Missenyi mkoani Kagera kimetoa wito kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla kuendelea kuidumisha amani kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.
Wametoa wito huo baadhi ya viongozi wa chama wakati wakizungumza na Radio Karagwe wakiwa ofisi za chama wilaya zilizopo kata Kyaka.
Viongozi hao akiwemo katibu wa jimbo Lauliani Kabakama amesema jamii ya paswa kuendelea kudumisha amani ya nchi kwa kuwa amani ndicho kitovu cha kila jambo na kwamba bila amani hapakaliki hivyo watu hawana budi kujiepusha na mambo yanayoweza kuvuruga amani wakitolea mfano wa baadhi ya maudhui yanayosambazwa mitandaoni yenye taarifa za uongo, uzushi na uchochezi.
Katibu Kabakama amefafanua kuwa kuna maisha baada ya siasa hivyo zinahitajika siasa safi ili kuyafikia malengo ya kuwachagua viongozi walio bora kupitia vyama vyote.

Naye Mwenyekiti wa ACT kata ya Kyaka mzee Jafari Ngemela Rwekaza amesema kwamba wamejipanga vizuri baada ya kufanya mikutano kadhaa wakimnadi mgombea udiwani kata ya Kyaka Bw. Daogratias Lauriani Kahwa na mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa hiyo ikiwa ni dalili ya ushindi kwa mgombea huyo.
Aidha amewatahadharisha wanasiasa kuacha mihemko na maneno yasiyofaa kwenye majukwaa ya mikutano kwani vyaweza kusababisha vurugu hatimaye kutoweka kwa amani iwe sasa na siku husika ya kupiga kura.