Karagwe FM

ACT Wazalendo yaahidi barabara na zahanati kata ya Mabale

19 September 2025, 12:56 pm

Mgombea nafasi ya udiwani kata ya Mabale jimbo la Missenyi Mhandisi Sweetbert Kaizilege John. Picha na Theophilida Felician

Uwepo wa changamoto katika kata mbalimbali katika jimbo la uchaguzi Missenyi mkoani Kagera imekuwa fursa ya wagombea kujinadi wakati wa kampeni za uchaguzi wakiahidi kutatua changamoto hizo endapo watachaguliwa kwa nafasi wanazosigombea

Na Theophilida Felician, Missenyi, Kagera.

Mhandisi Sweetbert Kaizilege John mgombea nafasi ya udiwani kata ya Mabale jimbo la Missenyi amesema kuwa amewania nafasi hiyo ili kuleta mabadiliko chanya na kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo yaliyokwama kwa muda mrefu.

Mhandisi Sweetberty amebainisha hayo akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni zake uliofanyika kitongoji cha Katweigiri kijiji cha Mabale na kuzitaja baadhi ya kero kuwa ni pamoja na changamoto ya barabara kutoka Kyaka, Kilimilile hadi kata ya Mabale.

Mgombea nafasi ya udiwani kata Mabale jimbo la Missenyi Mhandisi Sweetbert Kaizilege John

Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni uhaba wa zahanati kwani iliyopo haikidhi mahitaji kwa wananchi ukilinganisha na wingi wawatu wakata hiyo

Amehitimisha akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wanavyojitokeza kwa wingi kushiriki mikutano yake maeneo mbalimbali ya kata.

Naye Mgombea udiwani kata Kilimilile Danson Kasente naye akigombea kupitia chama cha ACT WAZALENDO akishiriki mkutano huo hakusita kuwaeleza wazi wananchi wa Mabale uchapakazi wa Mhandisi Sweetberty Kaizilege ambapo amewasihi wasimpoteze badala yake wamchague kwakishindo hatimaye Mabale isonge mbele kwani itakuwa imempata mtu sahihi katika suala zima la uajibikaji.

Mgombea udiwani kata ya Kilimilile kupitia chama cha ACT Wazalendo bw. Danson Kasente
Mkazi wa kitongoji cha Kigarama kijiji cha Makazi bi Zuraina Idd. Picha na Theophilida Felician

Bibi Zuraina Idd ni mkazi wa kitongoji cha Kigarama kijiji cha Makazi akimpongeza mgombea Sweetberty amemueleza kwamba katika kitongoji chao wanakabiliwa na changamoto ya wanyama waharibifu wa mazao ambao ni ngedere wanaoharibu mazao yao pamoja na changamoto ya maji hivyo amemuuomba atakapochaguliwa afanye jitihada za makusudi kuwanusuru na adha hiyo ambayo imewanyima usingizi muda mrefu.

Mkazi wa kitongoji cha Kigarama kijiji cha Makazi bi Zuraina Idd
Baadhi ya wananchi walihudhuria mkutano wa kampeni kata ya Mabale Missenyi