Karagwe FM

Kagasheki aahidi ujenzi wa soko Rwamishenye

6 September 2025, 7:54 pm

Mgombea udiwani kata ya Rwamishenye manispaa ya Bukoba kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Sued Juma Kagasheki. Piha na Theophilida Felician

Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Kagera kinaendelea na kampeni za kusaka udiwani ubunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali wakiahidi miradi ya maendeleo ikiwa wananchi wataendelea kukichagua

Theophilida Felician Bukoba.

Wafanya biashara wadogo kando ya barabara kuu ya kuelekea nchini Uganda kata Rwamishenye manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanatarajia kujengewa soko maalum ili kuondoa changamoto ya msongamano wa watu katika barabara hiyo.

Ametoa kauli hiyo mgombea udiwani kata ya Rwamishenye kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Suedi Juma Kagasheki akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kata hiyo.

Mgombea udiwani kata ya Rwamishenye kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw Sued Juma Kagasheki

Sued anayetetea kiti chake kwa mara nyingine tena amesema kwamba baada ya ongezeko la watu wanaofanya biashara barabarani serikali imeamua kuchukua hatua ya kulijenga soko litakalowasidia kuendesha biashara zao kwa huru na usalama.

Katibu wa CCM kata ya Rwamishenye Victor Baruan. Picha na Theophilida Felician

Viktor Baruan katibu wa chama kata pamoja naye Khalid Abudull mwenezi tawi la Rwamishenye wakimuombea kura Suedi Juma Kagasheki awali wameyaeleza mambo mbalimbali yenye maendeleo yaliyotekelezwa kupitia diwani huyo ikiwemo ya kuwatetea wananchi wanapokuwa na changamoto katika maeneo yao hususani soko la Rwamishenye ambapo mwenezi Khalidi ametolea mfano akina mama wauza samaki barabarani walivyokuwa wakiondoshwa eneo hilo hivyo alisimama kidete hatimaye akina mama hao waliendelea kubakia barabarani na biashara zao za uuzaji samaki.

Katibu wa CCM kata ya Rwamishenye Victor Baruan na Katibu wa uenezi tawi la Rwamishenye Khalid Abdul

Hata hivyo mgombea ubunge jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Johnston Mtasingwa akishiriki mkutano huo amesema ilani ya CCM ya mwaka 2025/ 2030 imesheheni miradi ya maendeleo ya kata ya Rwamishenye ambayo ni barabara za mitaa, ujenzi wa kituo kingine cha afya na soko la wafanyabishara wadogo wadogo.

Mgombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kwa tiketi ya CCM Mhandisi Johnston Mutasingwa
Baadhi ya makada wa CCM na wananchi walioshiriki mkutano. Picha na Theophilida Felician