Karagwe FM

Malalamiko 370 yapokelewa na EWURA CCC Kagera

4 September 2025, 2:44 pm

Afisa huduma kwa wateja wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera Anadorice Komba. Picha na Theophilida Felician

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera limeendeleza utamaduni wa kufuatilia kero za wananchi wanaotumia huduma hizo na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri na elimu kwa wananchi juu ya kutoa taarifa pale wanakumbwa na changamoto

Na Theophilida Felician, Kagera.

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC kwa upande wa mkoa wa Kagera limebainisha kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 limewafikia jumla ya watumiaji wa huduma hizo 16,496 na kupokea malalamiko 370.

Akitoa kauli hiyo afisa huduma kwa wateja mkoa wa Kagera Anadorice Komba katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera amesema kuwa wamefanikiwa kuwafikia wananchi hao kwa kutumia njia mbalimbali zilizowakutanisha pamoja na wananchi ikiwemo ya kushiriki matukio ya mikusanyiko hususani mikutano ya mitaa, matamasha likiwemo tamasha la Ijuka omuka, kuzifikia shule za msingi, sekondari na vyuo.

Afisa huduma kwa wateja wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera Anadorice Komba

Hata hivyo amewashukuru viongozi wote waliowapa ushirikiano katika maeneo na kuwaomba kuendelea namna hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Ametoa rai akiwasihi wananchi kuitumia ofisi ya EWURA CCC kwa kufika moja kwa moja ofisini ama kuwasiliana nao kupitia namba ya ofisi 0758829400 hiyo itawasaidia kuziwasilisha taarifa dhidi ya changamoto wanazozibaini katika utumiaji wa huduma za nishati na maji sambamba na kupata elimu ipasavyo.

Afisa huduma kwa wateja wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera Anadorice Komba