Karagwe FM
Karagwe FM
30 August 2025, 8:38 pm

Saulo mwenye elimu ya shahada ya kwanza katika sayansi ya usimamizi wa mazingira chuo kikuu cha kilimo Sokoine na shahada ya uzamili ya Sayansi ya afya ya jamii Muhimbili ameahidi kutumia elimu na uzoefu wake kuleta maendeleo ya wananchi wa Bukoba mjini mkoani Kagera
Na Theophilida Felician Bukoba.
Mgombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kupitia chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la Tumaini jema Bw Saulo Joseph Kamugisha amebainisha namna chama hicho kilivyojipanga kubadilisha maisha ya wananchi wa Bukoba kimaendeleo.
Saulo ameyasema hayo wakati akizungumza na Radio Karagwe Manispaa ya Bukoba amesema kuwa iwapo wananchi watampatia ridhaa ya kuliongoza jimbo atawajibika kiutendaji kwa lengo la kuinua na kuchechemua kasi ya maendeleo ili Bukoba iweze kusonga mbele
Aidha amevitaja vipaumbele vyao kama chama moja uchumi ulioboleka, elimu, maji, afya, uvuvi na miundombinu ya kijamii.
Hata hivyo ameeleza kuwa wana Bukoba hawana budi kubadilika na kuacha kupiga kura kwa mazoea na badala yake wachukue hatua stahiki kuwachagua viongozi bora ili wakayashuhudie mabadiliko makubwa kiutendaji hata miradi ya kimkakati inayojengwa jimboni humo ukiwemo wa soko kuu na barabara atahakikisha inakamilika kwa wakati.
Saulo mwenye elimu ya shahada ya kwanza katika sayansi ya usimamizi wa mazingira chuo kikuu cha sokoine na shahada ya udhamili ya sayansi ya afya ya jamii Muhimbili ana uzoefu katika ujenzi wa miradi ya maendeleo kupitia mashirika ya World Vision na Tumaini jema hivyo amewaomba wananchi wa bukoba kupitia vyama vyote kumuunga mkono na kumpa kura za kishindo.

Prosper Mbakile ni katibu wa CHAUMMA mkoa wa Kagera na mwenyekiti jimbo la Bukoba mjini amesema wamejipanga vizuri na kuwateua madiwani sambamba na wabunge wanne watakaoipeperusha bendera kupitia chama hicho ambayo ni Ngara, Biharamulo, Muleba kusini na Bukoba vijijini.
Katibu huyo amewahakikishia wananchi kuwa CHAUMMA imewateua wagombea imara na wazuri wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi iwapo watawaunga mkono na kuwachagua katika uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Oktoba 2025.