Karagwe FM
Karagwe FM
17 August 2025, 7:44 pm

Baadhi ya wajumbe wa chama cha ushirika Nguvu mali wilayani Karagwe wamejikuta katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha na kusababisha hasara kwa ushirika huo
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe
Wanachama wa chama cha ushirika wa Nguvu Mali wilayani Karagwe mkoani Kagera wameridhia kuwasimamisha wajumbe wawili wa bodi kutokana na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni mia tano uliochangia ushirika huo kupata hasara.
Akizungumuza na waandishi wa habari Agost 15. 2025 baada ya kumalizika mkutano wa dharura uliojumuisha baadhi ya wananchama wa ushirika wa nguvu mali katika kata ya Bugene, mwenyekiti wa ushirika huo Exavery France amesema kuwa wanachama baada ya kupokea taarifa ya afisa ushirika wilayani Karagwe iliyobainisha hasara iliyobainishwa katika ukaguzi wa ukusanyaji wa kahawa wajumbe wameridhia kuwasimamisha wajumbe wawili wa bodi hiyo wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu wa zaidi ya shillingi milioni mia tano.

Aidha kupitia katika mkutano huo wanachama wa ushirika wa Nguvu mali wamefanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wengine wa bodi baada ya bodi iliyokuwepo kuvunjwa na hapa afisa ushirika wilayani Karagwe Akwilina Meela ameimiza wajumbe hao wapya kufanya kazi kwa uadilufu baada ya kuaminiwa na wanachama.

Nao baadhi ya wajumbe wa bodi waliochaguliwa wamesema kuwa watahakisha wanafanya kazi kwa maslahi ya ushirika huku wajumbe waliosimamishwa wakikanusha kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo.