Karagwe FM

Viongozi TAMESOT wahani msiba wa mwasisi wao Kagera

6 August 2025, 6:47 pm

Katibu wa TAMESOT mkoa wa Kagera bw Patiani Kashubi. Picha na Theophilida Felician

Maisha ya mwanadamu ni kama maua yanayoweza kunyauka wakati wa jua, Hivi ndivyo unaweza kusema baada ya kusikiliza mkasa wa kifo cha mwasisi wa umoja wa waganga wa tiba asili mkoa wa Kagera aliyefariki ghafla hivi karibunu

Na Theophilida Felician Bukoba.

Wanachama cha waganga nchini TAMESOT mkoa Kagera wameshitushwa na kifo cha ghafla kilichomkuta mwaasisi wao Sadiki Nuru Hassan aliyekuwa akiishi katika mtaa wa Mkigusha kata ya Bilele manispaa ya Bukoba.

Baadhi ya viongozi wa chama hicho wameungana na dungu na wananchi kwa ujumla kumuombea dua marehemu Sadiki Nuru ambaye alikuwa nguzo muhimu kwa chama na tiba asili ambapo katibu wa chama mkoa Bw Patiani Kashubi kwa niaba ya viongozi wenzake baada ya kukabidhi rambirambi ya chama taifa na mkoa kwa familia amesema marehemu aliishi na kufanya kazi ya tiba asili kwa ushirikiano mkubwa.

Katibu Patiani amewasihi waganga wa tiba asili kuyaishi nakuyaiga mema yaliyotendwa na marehemu huyo enzi za uhai wake huku akitoa wito kuendelea kufanya kazi kwakuzingatia misingi na miongozo ya sekta hiyo kama yalivyo maelekezo ya serikali kwa lengo la kuziepuka changamoto wanazoweza kukabaliana nazo.

Katibu wa TAMESOT mkoa wa Kagera bw Patiani Kashubi
Bw. Ally Nuru Hassan, mdogo wake Marehemu.Picha na Theophilida Felician

Ally Nuru Hassan ni mdogo wa marehemu amesema kuwa Sadiki aliugua ghafla zikafanyika juhudi za kumpeleka hospitali ya Zamzam ambapo muda mfupi baadaye alikata roho wakati madaktari wakihangaika kufahamu ni ugonjwa gani uliomsumbua.

Bw. Ally Nuru Hassan, mdogo wake Marehemu

Amewashukuru TAMESOT kwa namna walivyokuwa nao kama familia tangu mazishi hadi kumuombea dua huku akiwaomba wazidi kuwa na utaratibu huo wa kusaidiana kama wanachama kwenye shida na raha.

Sheikhe wa wilaya ya Bukoba Yusuphu Kakwekwe (wa pili kulia). Picha na Theophilida Felician

Viongozi walioshiriki dua hiyo iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Buyekela kata ya Bakoba na kuongozwa na sheikhe wa wilaya ya Bukoba Yusuphu Kakwekwe ni pamoja naye mwenyekiti wa TAMESOT mkoa Halima Rwiza, mwenyekiti manispaa ya Bukoba Ally Mohamed Ally na Katibu wilaya Misenyi Ramadhani Rashidi pamoja na wanachama wengine kwa pamoja wameeleza kuwa kifo cha Sadiki Nuru ni pengo kubwa kwa tiba asili mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.