Karagwe FM

Wapiga ramuli chonganishi, sangoma wasiosajiliwa waonywa Kagera

29 July 2025, 8:23 pm

Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Adriano Modestusi (wa kanza kulia). Picha na Theophilida Felician

Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limeendelea kuonya dhidi ya vitendo vya waganga wanaopiga ramuli chonganishi sambamba na kuahidi kuchukua hatua waganga wasiosajiliwa

Na Theophilida Felician, Bukoba

Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limekishukuru na kukipongeza chama cha waganga wa tiba asili nchini TAMESOT kwa namna kilivyojizatiti kutoa elimu dhidi ya waganga wa tiba asili huku likiwaonya kutokushiriki ramuli chonganishi.

Ametoa kauli hiyo Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Adriano Modestusi kutoka ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Kagera wakati akifunga mafunzo ya TAMESOT kwa waganga yaliyofanyika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Amewaeleza waganga kuwa elimu waliyoipata ni muhimu kwao na itawasaidia kufanya kazi ya tiba kwa weledi, heshima pamoja na kuwaepusha kushiriki matukio yasiyofaa kwa jamii ikiwemo ramuli chonganishi.

Mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Adriano Modestusi
Katibu mkuu wa TAMESOT taifa Bw Lukas Joseph Mlipu (aliyesimama). Picha na Theophilida Felician

Katibu mkuu wa TAMESOT taifa Bw Lukas Joseph Mlipu akiwa mkufunzi wa mafunzo hayo awali amelishukuru jeshi la polisi mikoa yote anakopita ikiwemo Kagera limekuwa naye sambamba katika kumpa ushirikiano kwa vitendo kwani nalo limeshiriki moja kwa moja kutoa elimu na maelekezo madarasani na zoezi linaendelea vizuri maeneo yote.

Katibu mkuu huyo darasa lake limeyahusisha masomo mawili kutoka vitabu viwili vilivyolenga somo la miongozo kwa viongozi na somo la pili likiwalenga waganga wote kwa ujumla hakusta kutoa wito akiwataka waganga kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuwabaini watu wanaofanya kazi kinyume na utaratibu hususani matapeli ambao hushiriki matukio ya uhalifu.

Katibu mkuu wa TAMESOT taifa Bw Lukas Joseph Mlipu

Ziara ya kiongozi huyo pia inawahamashisha waganga kujitokeza wiki ya tiba asili ya mwafrika itakayofanyika Dodoma 25 hadi 31 Agost mwaka huu 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo. Picha na Theophilida Felician

Waganga ambao ni Adamu Kataga kutoka Muleba, John Shigera kutoka Missenyi, Mary Agustino manispaa ya Bukoba na katibu wa TAMESOT wilaya ya Misenyi bw.Ramadhani Rashidi wameshukuru kupata elimu iliyowapa mwanga wenye kuwajenga na kuwasaidia kufahamu mambo mbalimbali yanayoihusu tiba asili.

Baadhi ya waganga na viongozi wa TAMESOT walioshiriki mafunzo.