Karagwe FM
Karagwe FM
23 July 2025, 6:38 pm

Taasisi ya Ubalozi wa Amani Mkoa wa Kagera ni moja kati ya taasisi makini zinazoamini katika huduma bora baada ya kupata mafunzo maalum kuhusu mbinu za ulinzi wa amani nchini
Theophilida Felician
Wanachama wa taasisi ya ubalozi wa amani PPA mkoa wa Kagera wamepata mafunzo mbalimbali yanayolenga kutunza na kulinda amani.
Wanachama hao pia walijifunza moduli ya AMANI NA UZALENDO KATIKA JAMII pamoja na mambo muhimu yaliyomo ndani ya Moduli hiyo iliyoandaliwa na watalaamu wa taasisi hiyo.
Mada zilizohusika katika mafunzo yaliyofanyika katika manispaa ya Bukoba yamegusia viashiria na vyanzo vya uvunjifu wa amani ikiwemo ya malezi katika familia, kutokusimamia vyema misingi ya utawala bora katika jamii, upotoshwaji wa haki za binadamu, matumizi mabaya ya lugha na mapungufu katika utoaji mafunzo.
Wakifafanua vizuri darasani wakufunzi ambao ni Msabila Raphael, Justin Hassan Jackson wamesema mafunzo hayo yamelenga kuwaanda vyema mabalozi wa amani ili waweze kufanya kazi hiyo kwa weledi wanapopeleka elimu hiyo kwa jamii.
Vipengele hivyo vyenye viashiria vya uvunjifu wa amani vimeyagusia maeneo mengi ikiwemo ya malezi katika familia ambapo mkufunzi Msabila ametolea mfano hali ili kwa sasa katika kushuka kwakiwango cha maadili kwenye jamii na changamoto zake kuanzia ngazi ya familia na kuendelea.

Kwa ujumla wanadarasa wameyajadili mengi kulingana na malengo ya taasisi kama ambavyo mkurugenzi wa taasisi Maulid Rashidi na makamu mkurugenzi Mchungaji Venant Clavery walivyoeleza kuwa maadili yanayotakiwa ni ya kiroho na elimu kwa vitendo.
Naye mkufunzi Justin Hassan Jackson amewasisitiza wanataasisi wawapo majukwaani na maeneo mengine kuzingatia vipengele vya uvunjifu wa amani kama walivyojifunza.