Karagwe FM

Madeni, ugumu wa maisha chanzo watu kujiua Kagera

23 July 2025, 6:13 pm

Mchungaji wa kanisa la EAGT Mlima wa Ahadi Clavery Venant. Picha na Theophilida Felician

Wimbi la watu kujiua au mauaji dhidi ya watu wengine limeendelea kutikisa mkoa wa Kagera licha ya kuwa hakuna utafiti rasmi wa sababu za tatizo hilo.

Na Theophilida Felician, Bukoba

Maisha magumu, upweke, migogoro ya ndoa, wivu wa mapenzi, madeni makubwa, msongo wa mawazo, ulevi uliopindukia na ramli chonganishi ni miongoni mwa sababu zinazochangia kasi ya matukio ya watu kujitoa uhai kwa kujinyonga.

Kauli hiyo imetolewa na mchungaji wa kanisa la EAGT Mlima wa Ahadi Clavery Venant wakati akizungumza na Radio Karagwe ofisini kwake manispaa ya Bukoba na kusema kuwa kutokana na jamii kukabiliwa na changamoto mbalimbali watu wamekuwa wa kukata tamaa na matokeo yake kuchukua maamuzi yasiyo sahihi hususani ya kujiua matukio ambayo yameshika kasi kutokana na kuripotiwa mara kwa mara maeneo mbalimbali nchini.

Amefafanua kuwa kujiua siyo maamzi sahihi ni maamuzi mabaya kwani hali hii imepelekea athari ya kuwapoteza watu wanaoziacha familia zikitangatanga kwa jamii hasa watoto yatima.

Mchungaji wa kanisa la EAGT Mlima wa Ahadi Clavery Venant

Hata hivyo amewashauri viongozi wa dini, wanasaikolojia na makundi mengine kujitokeza na kuwasaidia wananchi kuwapa elimu yenye ufahamu juu ya madhara ya kujiua itaweza kuyapunguza na kuyadhibiti matukio ya namna hiyo kwa jamii