Katibu mkuu wa TAMESOT Lukas Joseph Mlipu, Picha na Theophilida Felician
Siku chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani Kagera kuwashikilia wanaume wawili ambao niKelvin Piason Mdolon (42), mkazi wa Mnyiha na mganga wa kienyeji pamoja na Randani Seme Mlomo (64), mkazi wa Mnyamwanga ambaye ni mtumishi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi, mkoa wa Songwe kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu, chama cha waganga wa tiba asili TAMESOT kimekuja na tamko kuhusu tukio hilo.
Na Theophilida Felician, Dodoma
Chama cha waganga wa tiba asili nchini TAMESOT kimetoa waraka mahsusi kwa serikali kufuatia tukio la kukamatwa kwa watu wawili wakiwa na viungo vya binadamu hivi karibuni mkoani Kagera.
Waraka huo uliotolewa na katibu mkuu wa TAMESOT Lukas Joseph Mlipu kutoka makao makuu ya ofisi za chama hicho zilizopo Kibaigwa mkoani Dodoma umevitaka vyombo vya upelelezi kama TAKUKURU, Jeshi la polisi na usalama wa taifa kuunda timu ya kuchunguza mtandao mzima wa uhalifu.
Pia imependekezwa kufungwa kwa waganga wa jadi wanaobainika kufanya kazi kwa kutumia viungo vya binadamu sambamba na jeshi la polisi kufanya msako kwa waganga wa jadi wasiokuwa na leseni za kuwaruhusu kufanya kazi ya tiba asilia.
Sambamba na hayo serikali imetakiwa kuwaunga mkono wenye taasisi zinazosimamia waganga zinazotoa elimu ya kuwajengea uwezo na uelewa waganga hao kwa lengo la kuwasaidia uelewa wa matumizi bora ya tiba asili.
WARAKA KWA SERIKALI NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU:- KUKAMATWA KWA MTU MKOANI KAGERA AKIWA NA VIUNGO VINAVYODHANIWA NI VYA BINADAMU NA VIFAA VYA MATAMBIKO.
UTANGULIZI TAMESOT TANZANIA ikiwa ni taasisi inayo jihusisha na Usimamizi na Utoaji Elimu Kwa Waganga wa tiba asili nchini na maadili ya tiba asili Kuelimisha jamii utofauti wa Waganga wa Jadi au Kienyeji Katika Tasnia yetu ya tiba asili hapa nchini Imesikitishwa na tukio la kukamatwa kwa mtu Mmoja mkoani Kagera akiwa na sehemu za siri za binadamu zilizokaushwa ambavyo ni mfupa wa taya, pembe za wanyama wa porini na viungo vingine vinavyodaiwa kutoka chumba cha maiti mkoani Songwe. Tukio hili linaibua maswali makubwa kuhusu usalama wa afya ya jamii, biashara ya viungo vya binadamu, ushirikina wa kisiasa na kiuchumi, na mtandao wa watu wanaokiuka haki za marehemu na maadili ya taifa.
MALENGO YA WARAKA HUU i. Kuishauri Serikali na vyombo vya dola kuhusu udhibiti wa matukio ya namna hii. ii. Kuwataka viongozi wa kisiasa, vyombo vya sheria, na taasisi za tiba asilia na jamii kwa ujumla kulaani matukio ya matumizi ya viungo vya binadamu. iii. Kutoa uchambuzi wa kisheria, kijamii na kiimani kuhusu tukio hili.
MAELEZO YA TUKIO KWA MUJIBU WA TAARIFA ZILIZOPO Mtu mmoja alikamatwa Kagera akiwa na: Sehemu za siri za binadamu zilizokaushwa Mfupa wa taya ya binadamu Pembe mbili za wanyama wa porini “Kondoo la mwanamke” – > mfuko wa uzazi, Anadai alivipata kutoka chumba cha maiti mkoani Songwe. Aidha, Mhudumu wa nyumba ya wageni aliweza kufahamu yaliyomo kwenye begi na kutoa taarifa, Jambo linaloibua maswali kuhusu usiri na mtandao wa ushiriki katika tukio. KIIMANI:-
Imani potofu kuhusu mafanikio: Kuna dhana inayopenya miongoni mwa baadhi ya wanasiasa au wafanyabiashara kuwa viungo vya binadamu vinatoa nguvu ya kutawala, kupata ushindi katika chaguzi mbalimbali, kupata mali (Kipato Kikubwa) aidha kinga ya kisiasa. Tameso T Tunasema hii ni imani potofu, isiyo na uhalisia wala siyo Misingi ya tiba ya asili yenye maadili.
Kuvunjwa kwa heshima ya marehemu: Katika imani za Tiba asili jadi Kienyeji , mwili wa marehemu unaheshimiwa. Aidha kuchukua viungo vya malehemu ni sawa na kufuru na matusi kwa Maadili ya Mizimu tunayoiamini waganga wa tiba asili na Watangulizi wetu waliotutangulia.
Viongozi wa waganga wa Tiba asili, kienyeji / Jadi waadilifu: Tunatoa wito kwa waganga wa jadi, na Jamii kwa Ujumla, na viongozi wa Makundi yote ya kijamii kulaani na kujitenga na aina hii ya Vitendo vya kichawi na vya kishirikina kwa Jamii, na Tuendelee kukemea Hasa kipindi hiki Cha Kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 ambapo Matukio haya hujitokeza kwa kuwa shirikisha Wana Siasa kwa kigezo Cha kuwapatia Madaraka. MADHARA KWA JAMII
Kupotea kwa maadili ya kitaifa: Tukio hili linaonyesha namna gani baadhi ya watu wameacha maadili na kujiingiza kwenye njia za Mkato za utajili na madaraka kwa njia zisizo halali, na Kwa Imani ya TAMESO Tananzania, Inakinzana Kwa asilimia 100% na vitendo hivyo vya kikatili vinavyofanywa na matapeli hao, aidha tunaishauli serikali wanapotiwa nguvuni wapewe adhabu kali kwani ni wauwaji kama wauwaji wengine. Pia TAMESO Tanzania tunasema hizo ni mbinu za Wanaotumia mwamvuli wa Tiba asili – Makutimakalauzinga na sio waganaga halisi kama jamii inavyo amini.
Athari kwa hofu ya raia: Matukio haya yanatishia amani, yanachochea hofu, na yanaharibu taswira ya Tasnia yetu ya Tiba asili hapa chini na Taswira ya waganga wa jadi kwa ujumla.
Uwezekano wa mtandao mkubwa wa kihalifu: TAMESO TANANZANIA Tunaamini kuwa haiwezekani mtu mmoja aweze kuiba viungo vya binadamu bila ushirikiano wa watu wengine kuanzia kwenye manunuzi katika hospitali, usafirishaji ikiwemo na wahitaji waliosababisha kufanyika kwa jambo hili hivyo tunaishauli serikali hasa jeshi la polisi yanapotokea matukio kama haya liweze kufuatilia mtandao mzima ili utiwe nguvuni na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. MAPENDEKEZO YA TAMESO TANANZANIA:
UCHUNGUZI MAALUMU WA KSEKTA: (inter – agency taskforce):
Vyombo vya upelelezi (TAKUKURU, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa) waunde timu kuchunguza mtandao mzima wa uhalifu huu.
Kufungwa kwa waganga wa jadi wanaotumia viungo vya binadamu:
Jeshi la polis kufanya Msako kwa waganga wa Jadi , Kienyeji wasiokuwa na lesseni za kuwaruhusu kufanya kazi zao.
Serikali iwaunge Mkono wenye Tasisi zinazowasimamia waganga wa tiba asili na zinazotoa Elimu ya kuwajengea uwezo na uelewa waganga wa tiba asili Jadi /Kienyeji ili kuepusha ufinyu wa elimu kwa tasnia hii ya tiba asili nchini na badala yake kuwa na uwelewa wa matumizi bora ya tiba asili hapa nchini. 5 Mapitio ya Sheria Na. 23 ya Tiba Asili ya mwaka 2002: Sheria hii ifanyiwe marekebisho ili iwe na adhabu kali dhidi ya waganga wachafu wanaochanganya tiba na uhalifu wa viungo na pia ishilikishe waganga watiba asili wenye uhalisia katika vikao vya ngazi zote vya maamuzi ikiwa ni pamoja na kuwa na msemaji katika bunge letu la jamuhuri ya muungano wa Tanzania. KAMPENI YA ELIMU KWA UMMA: Tameso T Tuanzishe kampeni za kitaifa kuelimisha Waganga wa Jadi/ Kienyeji na jamii kwa ujumla kuwa hakuna mafanikio ya kweli yanayopatikana kwa njia za kishirikina. TAMESO T tunaomba serikali, mashirika au wadau wanaoguswa na Tasnia hii ya tiba asili, watoe ruzuku ili kuiwezesha Tameso T kufanikisha kampeni hii yenye tija na kukomesha imani za kishirikina zinazopelekea mauwaji kwa jamii isio kuwa na hatia hapa nchini. HITIMISHO Tunaomba Serikali na vyombo vya habari kuchukulia tukio hili kwa uzito wa kiusalama, kiimani na kimaadili. Wakati umefika wa kutenganisha waganga wa jadi wa kweli na Makutimakalauzinga wanaofanya jinai kwa kisingizio cha kutoa huduma za tiba asili, aidha tunaiyomba jamii kwa ujumla iyelewe kuwa mganga wa tiba asili anatumia dutu za mimea, wanyama na sio kutumia viungo vya binaadamu. TAMESO Tanzania Tupo tayari kushirikiana na Serikali yetu tukufu na taasisi zote ili kuhakikisha jamii inalindwa na heshima ya binadamu inalindwa Kwa Maslahi mapana ya nchi yetu na kulinda Heshima ya Tasnia yetu ya tiba asili nchini: Imetolewa na: Lukas Joseph Mlipu Katibu Mkuu TAMESO T S L P 130 – Kibaigwa Dodoma: Email tamesottz@gmail.com