Karagwe FM

Mwenye ulemavu asiyeona atia nia ya udiwani Bukoba

2 July 2025, 9:55 pm

Mzee Novati Joseph Mwijage (wa pili kulia) akipokea fomu ya kugombea udiwani kata ya Bakoba. Picha na Theophilida Felician

Suala la wenye ulemavu kuacha kujinyanyapaa linaendelea kupigiwa kelele kwa kuwawezesha wenye ulemavu mbalimbali kushiriki katika fursa zinazojitokeza

Na Theophilida Felician, Bukoba

Changamoto ya ukosefu wa wawakilishi katika vyombo mbalimbali vya maamzi kwa kundi la watu wenye ulemavu limemsukuma mzee Novati Joseph Mwijage mwenye ulemavu asiyeona kujitosa na kuchukua fomu ya kuwania udiwani kata Bakoba manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Akichukua fomu hiyo kupitia chama cha mapinduzi CCM leo Tarehe 1, Julai 2025 katika ofisi za chama kata ya Bakoba amesema ni kwa kundi la watu wenye ulemavu mara kadhaa ili kuwa na uwakilishi wa kuwasemea changamoto zao bila ya mafanikio.

Sauti ya Mzee Novart Joseph Mwijage

Hata hivyo amewasihi watu wenye ulemavu kutokubakia nyumba badala yake wajitokeze na kuwania nafasi za uongozi kupitia vyama mbalimbali kwa lengo la kuwapata wawakilishi wengi kutokana na kundi hilo huku akiwaomba wananchi kuwaamini watu wenye ulemavu na kuwa chagua.

Aidha amewashukuru na kuwapongeza viongozi wa CCM kata ya Bakoba kwa namna walivyompatia ushirikiano katika zoezi zima la kuchukua fomu.

Alivinus Edward ni katibu wa CCM kata Bakoba amepongeza uthubutu wa mzee Novati akisema kuwa iwapo atafanikiwa nafasi ya kuwawakilisha wananchi kwenye baraza la madiwani itakuwa njia sahihi ya kuziwasilisha moja kwa moja changamoto za watu wenye ulemavu ili kufanyiwa kazi ya ufumbuzi.

Sauti ya katibu wa CCM kata ya Bakoba manispaa ya Bukoba bw. Alivinus Edward