Karagwe FM

RC Mwassa aitaka halmashauri ya Karagwe kumaliza hoja za CAG

18 June 2025, 1:38 pm

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa. Picha na Ester Albert

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewataka watumishi na watendaji wa halmashauri ya Karagwe kuendeleza juhudi zilizowawezesha kupata hati safi.

Na Ester Albert, Karagwe

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Karagwe kudumisha hati safi waliyopewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kuongeza uwajibikaji, ufanisi na kutekeleza mapendekezo wanayopewa na wakaguzi

RC Mwassa ameyasema hayo Juni, 17 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo (Angaza) mjini Kayanga wakati akihutubia kikao cha baraza la madiwani maalumu kilichoketi kujadili mapendekezo yaliyotolewa na CAG katika ugkaguzi wa hesabu ulioishia Juni 30.2024 na kutoa pongezi kwa halmashauri hiyo baada ya kupata hati safi.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa
Mkuu wa wilaya ya Karagwe (wa pili kushoto) wakati wa mapokezi ya mkuu wa mkoa wa Kagera wilayani Karagwe. Picha na Ester Albert

Naye, Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laizer amesema kuwa Halmashauri hiyo inajitahidi kupunguza madeni ya zamani na kuiomba serikali kuu kutenga bajeti ya kulipa madeni yanayodaiwa na mashirika ya umma kwa halmashauri hiyo ambapo hata hivyo mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Mwassa ameiagiza halmashauri kuweka watu maalum watakaohakiki fomu za wagonjwa kabla ya huduma katika vituo vya afya na hospitali.

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Mwassa
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda (katikati). Picha na Ester Albert

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Happines Msanga amesema kuwa halmashauri yake itatekeleza kwa weledi maelekezo yote ya mkuu wa mkoa huku mwenyekiti wa halmashauri ya Karagwe Wallace Mashanda akiwataka watumishi na mwadiwani kutobweteka na hati safi bali waendeleze ushirikiano.

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Karagwe Happines Msanga na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karagwe Wallace Mashanda