Karagwe FM
Karagwe FM
14 June 2025, 10:11 am

Magonjwa ya macho ni maradhi mbalimbali anayoweza kupata mtu na yakamtesa kama vile kisukari cha macho na glakoma (presha ya macho)
Na Jovinus Ezekiel
Zaidi wananchi 900 wilayani Karagwe mkoani Kagera wamenufaika na huduma ya matibabu bure ambayo imetolewa kwa muda wa siku nne katika hospitali ya wilaya ya Karagwe.
Akizungumza na wananchi waliofika katika hospitali ya wilaya ya Karagwe Nyakanongo kata ya Kayanga wilayani Karagwe kwa lengo la kupatiwa huduma ya matibabu ya macho bure, mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laizer ametoa shukurani kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ili wananchi wapate huduma ya matibabu kama walivyojitoa taasisi ya LaLji Foundation kuja wilayani Karagwe na kutoa huduma ya matibabu ya macho bure.

Katibu wa mbuge wa jimbo la Karagwe Ivo Ndisanye amesema kuwa huduma hii ni utekekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM katika uboreshaji wa huduma za afya kuwafikia wananchi kwa urahisi ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi ili wananchi wake wapate huduma.
