Karagwe FM

Vijana Karagwe waaswa kuchunguza wenza kabla ya kuoa

16 May 2025, 9:51 pm

Diwani wa kata ya Nyabiyonza Thomas Rwentabazi (mwenye kisemeo). Picha na Shabani Ngarama

Siku ya familia duniani wilayani Karagwe imeadhimishwa kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mambo kadhaa yanayowezesha ustawi wa familia

Na Shabani Ngarama, Karagwe

Afisa ustawi wa jamii wilayani Karagwe mkoani Kagera bi Owokusima Kaihura amewaomba vijana kuchunguza wenza kabla ya kuanzisha familia ili kupata watoto wenye maadili mema

Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Karagwe bi Owokusima Kaihura. Picha na Shabani Ngarama

Amesema hayo Mei 15.2025 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya familia yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Chabalisa kata ya Nyabiyonza na kusema kuwa familia nyingi huparaganyika baada ya wenza kushindwa kuelewana kwa sababu za toafuti za kimalezi walizozipata kwa wazazi wao

Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Karagwe bi Owokusima Kaihura
Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii bi Henrietha William. Picha na Shabani Ngarama

Kwa upande wake Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii bi Henrietha William ameitaka jamii kutokalia kimya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kuisaidia serikali kuchukua hatua dhidi ya wahusika wanaojihusisha na matukio hayo. Hata hivyo mtaalamu wa saikolojia na unasihi Hieronimo Rweyemamu aliyekuwa na mada kuhusu umuhimu wa kuandika wosia kuzuia migogoro ya mirathi mewataka wananchi kutunza siri kuhusu kilichomo katika wosia

Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Henrietha William pamoja na Mwanasaikolojia na mnasihi bw. Hieronimo Rweyemamu

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo diwani wa kata ya Nyabiyonza Thomas Rwentabaza aliyemwakilisha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe ameikumbusha jamii kuwa suala la malezi ya watoto si la mtu mmoja na kwamba mtoto wa jirani akiharibika ni jukumu la jamii kumrekebisha

Diwani wa kata ya Nyabiyonza Thomas Rwentabaza

Kauli mbiu ya siku ya familia duniani mwaka 2025 ni “Mtoto ni malezi, msingi wa familia bora, taifa imara”