Karagwe FM
Karagwe FM
24 April 2025, 6:47 pm

Serikali kupitia idara ya afya mkoani Kagera imefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria licha ya baadhi ya wilaya kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi
Theophilida Felician.
Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa mkoa wa Kagera kimepungua kutoka 34.9% mpaka 29.4% kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu wa 2025 licha ya maambukizi kupanda kwa wilaya za Ngara, Biharamulo na Kyerwa.
Akisema hayo mratibu wa maleria mkoa wa Kagera katika hospitali ya rufaa Bukoba Dr Carlos Christian amesema kuwa jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika mapambano dhidi yakuutokomeza ugonjwa huo.
Amefafanua kwamba kiwango cha maambukizi zaidi ni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ukilinganisha na makundi mengine ambapo mambukizi kwa wilaya ya Ngara yanaongoza kwa 51.5% Biharamulo 36.6% Kyerwa 34.9% na Bukoba DC 29.6%.
Aidha amezitaja jitihada zilizopelekea kupungua kwa maambukizi nipamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maleria kupitia njia tofautitofauti ikiwemo ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii, vyombo vya habari kupewa dawa kinga wananchi, vyandarua na mengineyo na kwamba vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimepungua ukilinganisha na mwaka jana wa 2024.
Amesisitiza kuwa mapambano dhidi malaria ni ya watu wote hivyo wananchi yawapasa kuendelea kuzingatia maelekezo ya watalaamu ili kujikinga na maambukizi huku akiwahimiza kuwahi vituo vya kutolea huduma ya afya wanapohisi kuwa na dalili za maleria.