Karagwe FM

I.P.I yalaani kitendo cha Mchungaji Kelvin kutoa baraka kwa kipigo

17 April 2025, 3:46 pm

Viongozi wa dini barani Afrika wamekuwa kimbilio la viongozi wa serikali kuwaomba kuhubiri na kulinda amani hasa zinapowadia nyakati za chaguzi. Hali imekuwa tofauti nchini Uganda ambapo nabii mmoja ametuhumiwa kuhatarisha amani ya nchi kwa kutembeza kichapo kwa waumoni wakiwa kanisani bila kujali hadhi, jinsi au umri wa mtu.

Theophilida Felician, Dar es Salaam.

Taasisi inayojishughulisha na utoaji elimu ya amani hapa nchini, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla INTERNATIONAL PEACE INFORMATION I.P.I imelaani tukio la mchungaji Kelvin wa nchini Uganda kuwachapa viboko waumini wake kanisani kwa madai ya kuwapa baraka.

Akitoka kauli ya masikitiko juu ya tukio hilo Rais wa I.P.I akiwa na viongozi wenzake ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Manispaa ya Temeke Dare es Salaam Prof Wilson George Munguza amesema tukio hilo ni la udhalilishaji na halikubaliki kamwe kwenye jamii.

Amefafanua kwamba baada ya kuona vyombo vya habari vikiripoti tukio hilo zikiwemo vidio zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii limewashangaza na kuwasikitisha kwani kufanya hivyo ni sehemu ya viashiria vya uvunjifu wa amani.

Rais wa taasisi ya I.P.I Prof. Wilson George Munguza

Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani hususani hapa nchini kuendelea kuwa makini ili viongozi wa dini kama Kelvin wasipate upenyo wakuendesha maovu yao kwa wananchi kama ilivyokwishafanywa kwa nabii mchawi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) aliyefukuzwa baada ya kwenda kinyume na utaratibu.

Amehitimisha akisisitiza kuwa wao kama taasisi maeneo yote watashirikiana na serikali kufichua uhalifu wa aina yoyote unaoweza kusababisha uvunjifu wa amani.