Karagwe FM

Askofu Munguza akemea rushwa na udini wakati wa uchaguzi mkuu

7 April 2025, 6:28 pm

Askofu mkuu wa makanisa ya Restoration of Power Ministry Prof. Wilson George Munguza. Picha na Theophilda Felician

Kila unapokaribia wakati wa uchaguzi huibuka hofu ya mambo mbalimbali yanayoweza kuvuruga uchaguzi ikiwemo ukabila, udini na vitendo vya rushwa

Na Theophilida Felician.

Askofu mkuu wa makanisa ya Restoration of Power Ministry Prof. Wilson George Munguza amewaasa viongozi wa dini nchini kusimama imara katika kuyakemea mambo mbalimbali yakiwemo ya rushwa na udini hususani nyakati hizi za kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Askofu Munguza akitoa kauli hiyo akiwa katika kanisa la Miji na Vijiji lililopo kata Toangoma mkoani Dar es Salaam ameeleza kwamba vipindi vya michakato ya chaguzi hujitokeza mambo mengi baadhi yake yakiwa hayafai hivyo ni wajibu wao kama viongozi wa dini kupaza sauti mapema ili kuyadhibiti.

Askofu mkuu wa makanisa ya Restoration of Power Ministry Prof. Wilson George Munguza

Hata hivyo ameipongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inavyoongoza kwa kuwaunganisha watu pamoja ili kuijenga nchi kwa umoja huku akiiomba kuwa macho na kuwachukulia hatua wanasiasa watakaobainika kwenda kinyume kwakukiuka misingi na kanuni za uchaguzi.

Askofu mkuu wa makanisa ya Restoration of Power Ministry Prof. Wilson George Munguza