Karagwe FM
Karagwe FM
5 April 2025, 5:53 pm

Kumekuwepo malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kutozwa fedha na wenyeviti wa vijiji na vitongoji ili wawasainie nyaraka na kuwagongea mhuri wa serikali kote nchini
Na Respicius John, Missenyi Kagera
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoa wa Kagera Bw. John Paulo Wanga amepiga marufuku matumizi ya mihuri ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji kutumika katika nyaraka mbalimbali wanazosaini na badala yake itumike mihuri ya maafisa watendaji wa vijiji na kata
Wakili Wanga ametoa marufuku hiyo wakati wa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa serikali za mitaa wilayani yakilenga kuongeza uwezo na ufanisi katika maeneo yao ya kazi

Nao baadhi ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji wameunga mkono marufuku hiyo wakisema kuwa upigaji wa mihuri katika nyaraka kulikuwa kukiwachonganisha na wananchi