Karagwe FM
Karagwe FM
31 March 2025, 9:17 pm

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bunazi Bonde la Baraka wilayani Missenyi limeendesha harambee kwa lengo la kukusanya shilingi milioni 100 za awali kwa ajili ya ujenzi wa kanisa linalotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 900
Na Respicius John, Missenyi-Kagera
Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali mstaafu Hamis Mayamba Maiga amechangisha zaidi ya shilingi milioni 28 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bunazi Bonde la Baraka
Katika harambee ya kuchangia ujenzi iliyofanyika Machi 30. 2025 Mchungaji wa Kanisa hilo Mwesiga Rushoke amesema kuwa zinahitajika shilingi milioni 900 kukamilisha ujenzi na kwamba gharama za msingi pekee ni shilingi milioni 100

Mchungaji Rushoke amesema kuwa ujenzi wa Kanisa jipya unafuatia Kanisa la zamani walilokuwa nalo kujaa maji yaliyosababishwa na mafuriko ya mvua iliyonyesha mwaka 2023 nakusababisha baadhi ya majengo katika mji wa Bunazi kuathirika likiwemo kanisa hilo
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Mstaafu Hamis Mayamba Maiga aliyekuwa mgeni rasmi ameongoza wageni waalikwa na waumini katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa kwa awamu ya kwanza ambapo jumla ya shilingi milioni 28 zimepatikana kati ya shilingi milioni 100 zilizolengwa kwa ajili ya kujenga msingi wa jengo

Kwa Upande wake Baba Askofu Joas Baganda kanisa la Nazareth Assemblies of God Nchini amewaomba waumini na wananchi wengine kuendelea kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kwakuwa zama za kupata ufadhili kutoka nje zimekwisha kwasasa hawahitaji wazungu kuchangia badala yake Kanisa linategemea waumini wake kulijenga na siyo wazungu ambapo pia baada ya zoezi la harambee kukamilika kanali mstaafu Maiga ametangaza kupatikana zaidi ya shilingi milioni 28